AFRIKA KUSINI-KASHFA-ZUMA

Jacob Zuma aepuka mashtaka ya rushwa

Jumatatu hii Mei 23 asubuhi, Ofisi ya mashtaka imeamua kutozingatia karibu mashtaka 800 yarushwa dhidi ya Jacob Zuma. Uamuzi huu wa Ofisi ya mashtaka unakwenda kinyume na uamuzi wa Mahakama Kuu ya mjini Pretoria, ambayo mwezi uliopita ilitoa uamuzi kuwa tuhuma dhidi ya Rais Zuma zinapaswa kuzingatiwa.

Ofisi ya mashtka ya imefutilia mbali mashitka ya rushwa dhidi ya Jacob Zuma.
Ofisi ya mashtka ya imefutilia mbali mashitka ya rushwa dhidi ya Jacob Zuma. REUTERS/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Kesi hii ya mkataba wa silaha ingelizingatiwa, bila shaka ingelimdhoofisha zaidi rais Zuma katika mazingira ya kisiasa na kiuchumi yanayoendelea kukabili.

Aprili 29, Mahakama Kuu ya mjini Pretoria iliamua "kutozingatia" uamuzi wa Ofisi ya mashtaka wa kufutilia mbali, mwaka 2009 kwa mfumo wa kiutaratibu, mashtaka 783 dhidi ya rais wa sasa wa Afrika Kusini na kubaini kwamba unapaswa kurejelewa "upya" .

"Zuma anapaswa kufuatliwa kwa mashtaka haya," aliongeza jaji wa Mahakama Kuu ya mjini Pretoria, Aubrey Ledwaba, ambaye aliombwa nachama kikuu cha upinzani cha DA (Democratic Alliance).

Njia nyingi mbadala zinawezekana: Ofisi ya mashtaka inaweza kuzingatia jumla au sehemu ya mashtaka 783 dhidi ya Zuma, au kuamua kukata rufaa hukumu ya Mahakama Kuu.

Mashtaka ya kashfa ya rushwa yanahusishwa katika mkataba mkubwa wa dola bilioni 4.8 ulioafikiwa mwishoni mwa miaka ya 90 na serikali ya Afrika Kusini pamoja na makampuni kadhaa, ikiwa ni pamoja kampuni ya Ufaransa Thomson-CSF (ambayo kwa sasa inaitwa Thales), kampuni ya Sweden Saab na kampuni ya Uingereza BAE Systems.

Mwezi Desemba 2007, Jacob Zuma, wakati huo kiongozi wa chama tawala cha ANC )African National Congress), alishtakiwa kwa kashfa ya rushwa, ukwepaji wa kodi na kujihusisha katika kesi isiyomhusu. Alishutumiwa kukubali kupokea hongo kutoka makampuni ya kimataifa ya kutengeneza silaha.

Lakini mashtaka yalifutwa ghafla, wiki tatu kabla ya uchaguzi wa mwaka 2009 uliyompelekea Jacob Zuma kchukuahatamu ya uongozi wa nchi.