DRC-UN-UCHAGUZI

UN: "uchaguzi kufanywa kwa muda uliopangwa na katiba inawezekana DRC"

Kinshasa, 3 Desemba 2011. Mjumbe wa tume ya Uchaguzi (CENI).
Kinshasa, 3 Desemba 2011. Mjumbe wa tume ya Uchaguzi (CENI). © AFP / Gwenn Dubourthoumieu

Ripoti ya siri ya wataalam wa Umoja wa Mataifa imebaini kuwa upo uwezekano wa kufanya uchaguzi nchini jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ndani ya muda uliopangwa kikatiba.

Matangazo ya kibiashara

Watalaam wanasema kuwa ni lazima hatua zote zifanyike ili kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unafanyika.

Kwa upande wake Tume ya Uchaguzi, imesema kwa sasa haiwezekani uchaguzi kufanyika kwa muda uliopangwa kikatiba. "Wataalam wa Umoja wa Mataifa wanasema hayo kwa sababu wao hawataki kwenda kinyume na azimio lao- ambalo linatoa wito wa kuheshimu muda uliopangwa kikatiba," vyanzo vya Tume ya uchaguzi vimesema, na kuongezakuwa, "wao wametaka tu kutoa ripoti yao, ili kuonyesha kama inawezekana wakati si vyo. Kwa nini ripoti hiyo wameiweka siri? "

Kwa upande wa wataalam wa Umoja wa Mataifa, bila marekebisho ya daftari la wapiga kura, bado inawezekana kufanyika kwa uchaguzi kwa muda uliopangwa

Kwa upande wa CENI, hata bila ya kupitia upya daftari la wapiga kura, uchaguzi wa rais unaweza kufanyika mwezi Aprili 2017. "Kwa nini ripoti hiyo haitangazwi rasmi? Wanakataa kushtumiwa kuwa wamekiuka katiba, " vyanzo vya Tume ya Uchaguzi vimebaini.

Duru zinasema, huenda tume ya uchaguzi ikaanda uchaguzi wa urais mwezi Aprili mwaka ujao.