Vyombo vya sheria kuamua kama vitamfuatilia Zuma
Imechapishwa:
Ofisi ya mashtaka ya Afrika Kusini itatangaza Jumatatu hii kama itazingatia au la mashataka 800 ya kashfa ya rushwa dhidi ya Jacob Zuma katika kesi ya mkataba wa silaha, tukio ambalo linaweza kumdhoofisha zaidi rais katika mazingira ya kisiasa na kiuchumi yanayoendelea kukabili.
Aprili 29, Mahakama Kuu ya mjini Pretoria iliamua "kutozingatia" uamuzi wa Ofisi ya mashtaka wa kufutilia mbali, mwaka 2009 kwa mfumo wa kiutaratibu, mashtaka 783 dhidi ya rais wa sasa wa Afrika Kusini na kubaini kwamba unapaswa kurejelewa "upya" .
"Zuma anapaswa kufuatliwa kwa mashtaka haya," aliongeza jaji wa Mahakama Kuu ya mjini Pretoria, Aubrey Ledwaba, ambaye aliombwa nachama kikuu cha upinzani cha DA (Democratic Alliance).
Kwa sasa uamuzi uko miikononi mwa Ofisi ya mashtaka, ambayo itaamua Jumatatu hii katika mkutano na waandishi wa habari mjini Pretoria.
"Ofisi ya mashtaka imetakiwa hadi Jumatatu iwe imechukua uamuzi wake (...) Itatangaza uamzi huo katika mkutano na vyombo vya habari saa 4 asubuhi saa za Afrika Kusini (sawa na saa 2 asubuhi saa za kimataifa)," msemaji wa Ofisi ya mashtaka, Luvuyo Mfaku, ameliambia shirika la habari la AFP.
Njia nyingi mbadala zinawezekana: Ofisi ya mashtaka inaweza kuzingatia jumla au sehemu ya mashtaka 783 dhidi ya Zuma, au kuamua kukata rufaa hukumu ya Mahakama Kuu.
Mashtaka ya kashfa ya rushwa yanahusishwa katika mkataba mkubwa wa dola bilioni 4.8 ulioafikiwa mwishoni mwa miaka ya 90 na serikali ya Afrika Kusini pamoja na makampuni kadhaa, ikiwa ni pamoja kampuni ya Ufaransa Thomson-CSF (ambayo kwa sasa inaitwa Thales ), kampuni ya Sweden Saab na kampuni ya Uingereza BAE Systems.
Mwezi Desemba 2007, Jacob Zuma, wakati huo kiongozi wa chama tawala cha ANC )African National Congress), alishtakiwa kwa kashfa ya rushwa, ukwepaji wa kodi na kujihusisha katika kesi isiyomhusu. Alishutumiwa kukubali kupokea hongo kutoka makampuni ya kimataifa ya kutengeneza silaha.
Lakini mashtaka yalifutwa ghafla, wiki tatu kabla ya uchaguzi wa mwaka 2009 uliyompelekea Jacob Zuma kchukuahatamu ya uongozi wa nchi.