ERITREA-UHURU

Eritrea yaadhimisha miaka 25 ya uhuru

Mji wa Eritrea, Asmara.
Mji wa Eritrea, Asmara. © REUTERS/Thomas Mukoya

Eritrea inaadhimisha Jumanne hii, Mei 24, miaka 25 ya uhuru wake. Mei 24, 1991, waasi wa Ethiopia waliudhibiti mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, wakati ambapo katika mji mkuu wa Eritrea, ambao ulikuwa bado mkoa wa Ethiopia, ndugu zao wa Eritrea walikua wakivitimua vikosi vya mwisho vya dikteta Mengistu.

Matangazo ya kibiashara

Miaka miwili baadaye, kura ya maoni nchini Eritrea ilipigwa na na kupata uhuru, baada ya miaka 30 ya vita vya maguguni. Leo hali ni tofauti sana katika mji wa Asmara. Sherehe zimepangwa kwa uhakika ili kusherehekea siku hii ambayo ni muhimu sana kwa wananchi na viongozi wa Eritrea, nchi ndogo ya Pembe ya Afrika ambayo vijana wake wengi wamekusanyikia katika miji mbalimbali ya nchi hiyo tangu miaka kadhaa iliyopita kwa kutafuta ajira.

Bendera ya taifa hilo itawekwa kila mahali katika mji wa Asmara siku ya leo. Ni miaka 25 sasa tangu Eritrea ijikomboe kutoka mikononi mwa jeshi la Ethiopia, lililokua likiongozwa na dikteta Mengistu.

Hata hivyo utawala wa Eritrea umekua ukilaumiwa kwa ukandamizaji ambao umekua ukiendeshewa wapinzani na raia wanaothubutu kupinga utawala wa rais Issayas Afeworki, ambaye alikua kiongozi wa vita katika harakati za kulikomboa taifa hilo kutoka mikononi mwa dikteta Mengistu na majeshi yake. Vyama vya kiraia vimekandamizwa na jela zimejaa wafungwa, wengi wao wakiwa ni wafungwa wa kisiasa. Robo ya idadi ya raia wa Eritrea waliikimbia nchini hiyo miaka ya hivi karibuni.

Ukandamizaji wa kisiasa umesababisha raia wengi hasa vijana. Lakini licha ya shinikizo kutoka jumuiya ya kimataifa, Rais Afeworki ameendelea kufumbia macho tuhuma dhidi yake.

Leo, hotuba ya kiongozi wa zamani wa vita, ambaye ni rais wa sasa wa Eritrea, imejikita katika mambo matatu, ikiwa ni pamoja na njama za kimataifa zenye lengo la kuchochea uhasama baina ya raia wa Eritrea, uhamasishaji muhimu wenye kudumu kwa wananchi na mafanikio ya kuvutia ya serikali yake katika mazingira ya uadui uliokithiri.

Kwa sasa Eritrea ni nchi ya kwanza yenye wakimbizi wengi barani Afrika