UNSC-SUDAN

UNSC kujadili uwezekano wa kuongeza muda wa majeshi yake Sudan

Askari wa kulinda amani wa UNAMID kaskazini mwa Darfur, Julai 5, 2010.
Askari wa kulinda amani wa UNAMID kaskazini mwa Darfur, Julai 5, 2010. AFP/ASHRAF SHAZLY

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wiki ijayo litaanza mazungumzo ya kuwaongezea muda vikosi vya kulinda amani katika jimbo la Darfur nchini Sudan.

Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya wanajeshi 20,000 kutoka mataifa 30 wamekuwa wakilinda amani tangu mwaka 2007.

→ (Soma zaidi) : Sudan haiko tayari UN kuongeza muda wa kikosi chake

Sudan imesema haitaomba Jumuiya ya Kimataifa kuwaongezea muda zaidi vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa vinavyohudumu katika jimbo la Darfur baada ya muda wao kukamilika mwezi Juni.

Wizara ya Mambo ya nje imesema hali ya utulivu imeshaanza kurejea katika jimbo hilo na raia wanasema wako salama na hivyo hakuna haja ya kuendelea kuwepo kwa wanajeshi wa Umoja wa Mataifa.