DRC: upinzani waruhusiwa kufanya maandamano Kinshasa
Imechapishwa:
Mkuu wa mji wa Kinshasa hajapinga maandalizi ya maandamano ya muungano wa vyama vya upinzani Alhamisi hii, Mei 26 katika mji mkuu wa Congo, Waziri wa Mambo ya Ndani katika mkoa wa Kinshasa, Emmanuel Akweti ametangaza, katika mkutano na wajumbe wa muungano wa upinzani.
Hata hivyo muungano huo wa vyama vya upinzani umekemea kwa mara nyingine tena uamuzi wa Mahakama ya Katiba, ambayo inamruhusu Rais Joseph Kabila kubaki madarakani iwapo uchaguzi hautofanyika mwaka 2016
Kwa sasa maandamano ya muungano wa vyama vya upinzani yameruhusiwa katika mji wa Kinshasa.Tayari mabadiliko fulani yameanza kuonekana iwapo maandamano hayo yatafanyika Alhamisi wiki hii. Hii ni sehemu ya majukumu ya serikali za mikoa kwa mujibu wa Katiba na sheria, amesema Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama.
Mkutano ulidumu karibu masaa mawili mbele ya mkuu wa mji wa Kinshasa na baraza lake la mawaziri, mkuu wa polisi wa mkoalakini pia ujumbe wa ngazi ya juu wa tume ya Umoja wa mataifa nchini Congo (MONUSCO) uliyofuata mijadala. Muungano wa vyama vya upinzani kupitia Wakili Poela, mratibu wake, aliishukuru hasa polisi na ujumbe wa Umoja wa Mataifa. "Hakuna haja ya kuwa na mashaka. Maandamano yameruhusiwa, " Wakili Poela, amesisitiza.
Mikusanyiko imepigwa marufuku mahali pengine nchini
Katika maeneo mengine ya nchi, hata hivyo, maandamano ya upinzani yamepigwa marufuku, kama katika mji wa Lubumbashi na Mbuji Mayi, ambapo viongozi wamesema hayana umuhimu wowote.
Katika mkutano na waandishi wa habari, mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini, Julien Paluku amepiga marufuku maandamano katika maeneo yote ya mkoa huo.