AFRIKA KUSINI-SHERIA

Bunge la Afrika Kusini lapitisha muswada wa sheria ya ardhi

Shamba la mahindi Afrika Kusini.
Shamba la mahindi Afrika Kusini. Waldo Swiegers/Bloomberg via Getty Images

Bunge nchini Afrika Kusini limepitisha muswada wa sheria unaoruhsuu serikali kutumia ardhi ya nchi hiyo kwa maslahi ya wananchi wa taifa hilo.

Matangazo ya kibiashara

Hii inamaanisha kuwa raia weusi nchini humo watakuwa katika nafasi nzuri ya kununua na kumiliki ardhi kinyume na ilivyokuwa hapo awali.

Chama tawala cha ANC nchini Afrika kusini kimepongeza kura iliyopigwa na bunge la taifa hilo, ya kuipa serikali mamalaka ya kutwaa ardhi yoyote kwa maslahi ya umma.

ANC inasema sheria hiyo itawapa haki raia wengi wa taifa hilo waliopokonywa mashamba yao.

Hata hivyo, chama cha Democratic Alliance ambacho kina wazungu wengi kimepinga mswada huo ambao tayari umekuwa sheria baada ya kutiwa saini na rais Jacob Zuma.