COTE D'IVOIRE-SIMONE

Mahakama kuu yafutilia mbali rufaa ya Simone Gbagbo

Simone Gbagbo akiwasili mahakamani  Abidjan, Jumatatu, Februari 23, 2015.
Simone Gbagbo akiwasili mahakamani Abidjan, Jumatatu, Februari 23, 2015. AFP/ISSOUF SANOGO

Mahakama ya Juu nchini Côte d’Ivoire, imekataa rufaa ya Simone Gbagbo, mke wa rais wa zamani wa nchi hiyo Laurent Gbagbo baada ya kuhukumiwa jela miaka 20 kwa kuchochea na kufadhili machafuko ya baada ya Uchaguzi mkuu mwaka 2010.

Matangazo ya kibiashara

Wakili wake, Rodrigue Dadje amesema uamuzi wa Mahakama kukataa rufaa hiyo umechochewa kisiasa.

Simone, alihukumiwa mwezi Machi mwaka huu pamoja na watu wengine 78 lakini hadi kuhukumiwa kwake, alikanusha kuhusika.

Mumewe, Laurent Gbagbo ameshatakiwa katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC mjini Hague nchini Uholanzi.