COTE D'IVOIRE-BURKINA FASO-MAUAJI

Mashambulizi ya Grand-Bassam: mmoja wa wahusika akamatwa Abidjan

Askari wa Côte d’Ivoire katika mji wa Grand-Bassam, Machi 13, 2016, siku ya shambulio.
Askari wa Côte d’Ivoire katika mji wa Grand-Bassam, Machi 13, 2016, siku ya shambulio. © REUTERS/Luc Gnago

Mmoja wa wahusika wa mashambulizi yaliyotekelezwa katika mji wa mapumziko wa Grand-Bassam mwezi Machi 2016 na kugharimu maisha ya watu 19, alikamatwa Alhamisi 26 Mei katika mji wa Abidjan. Kwa mujibu wa taarifa za awali, mtu huyo aliendesha gari aina ya Toyota 4x4 iliyosafirisha silaha zilizotumiwa na magaidi.

Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya usalama vya Côte d’Ivoire vilimkamata Barry Battesti katika kata ya Kumasi, kusini mwa mji wa Abidjan, karibu saa 7 mchana Alhamisi hii, Mei 26. Kukamatwa kwake kuliwashangaza wengi. Barry Battesti aliyekimbilia mafichoni, ambaye anashtumiwa kuendesha gari aina ya Toyota 4x4 hakuonyesha upinzani kwa kukamatwa kwake. Uraia wa barry Battesti, mwenye umri wa miaka 24 haujafanyiwa kazi kwa uhakika, lakini inasadikiwa kuwa alizaliwa nchini Côte d’Ivoire.

Ushahidi wa kwanza wa uchunguzi: gari ya aiana ya Toyota 4x4 ilitumiwa kwa kusafirisha silaha na baadhi ya magaidi katika mji wa mapumziko wa Grand Bassam tarehe 13 Machi. Wachunguzi waliweza kuweka wazi barabara ambazo gari ilitumia.

Novemba 11, gari hiyo aian ya Toyota 4X4 iliondoka katika mji wa Bamako kwenda Côte d’Ivoire. Baada ya kupita katika mji wa Dabou, ilitumia barabara inayoelekea Burkina Faso hadi katika mji wa Ouagadougou Januari 9. Siku sita baadaye, hoteli ya Splendid na mgahawa wa Cappuccino vilishambuliwa.

Kukamatwa kwa Barry Battesti ni tukio kubwa kwa mamlaka ya Côte d’Ivoire, kwa sababu katika uwezekano wowote ni moja ya viungo muhimu katika mzunguko wa magaidi. Kama ushahidi, yeye na Kunta Dalla walipigiana simu na mtu mwengine ambaye anaweza kuwa mtu muhimu wa mashambulizi ya mjini Ouagadougou na Grand-Bassam. Uhusiano huu unaonyesha kuwa kuna uwezekano kuwa mashambulizi nchini Burkina Faso na Côte d’Ivoire yalitekelezwa na timu moja ya magaidi.