Kanisa Katoliki lamtaka Kabila kuzungumzia hali ya usalama
Imechapishwa: Imehaririwa:
Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wanamtaka rais Joseph Kabila kujitokeza na kuzungumzia hali ya kisiasa na usalama nchini humo.
Kanisa Katoli linasema, huu ndio wakati wa kumsikia kiongozi wa nchi hiyo ili kutoa mwelekeo wa kisiasa nchini humo wakati huu kukiwa na hali ya wasiwasi ikiwa uchaguzi wa urais utafanyika mwaka huu au la.
Kauli hii inakuja siku kadhaa baada ya wapinzani kuandamana jijini Kinshasa na Mashariki mwa nchi hiyo kushinikiza kufanyika kwa uchaguzi lakini pia kupinga uamuzi wa Mahakama kuwa rais Kabila anaweza kuendelea kuwa madarakani hata kama uchaguzi hautakuwepo mwaka huu.
Masharika ya kiraia nchini humo yanasema hatua ya Maaskofu hao ni sahihi , na yamebaini kwamba yanaunga mkono wito huo