UBELGIJI-HABRE

Ubelgiji yakaribisha hukumu dhidi ya Habre

Serikali ya Ubelgiji ambayo ilikuwa ya kwanza mwaka 2005 kutowa waranti ya kimataifa ya kukamatwa kwa rais wa zamani wa Tchad Hissene Habre, imesema kwamba imeridhishwa na maamuzi ya mahakama maalum ya Afrika.

Hissene Habre akizungukwa na wanajeshi baada ya kusikilizwa, Julai 2, 2013, Dakar.
Hissene Habre akizungukwa na wanajeshi baada ya kusikilizwa, Julai 2, 2013, Dakar. © .AFP/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Mahakama hiyo ilimuhukumu Jumatatu wiki hii kiongozi huyo kifungo cha maisha jela kutokana makosa ya uhalifu dhid ya binadamu na makosa ya kivita.

Kwa mujibu wa taarifa ya waziri wa mambo ya nje wa Ubelgiji Didier Reynders, ameipongeza Senegal na kueleza kuwa huu ni mfano wa kuigwa na ni ujumbe kwa viongozi wengine waliopo madarakani na ambao hutumia vibaya madaraka yao.

Akisoma hukumu hiyo baada ya kusikiliza kwa muda waa saa moja, jaji Gberdao Gustave Kam, amesema Mahakama imemuhukumu kifungo cha maisha, uamuzi ambao umepokelewa kwa nderemo na vifijo.

 Hii ni hukumu ya kwanza kutolewa duniani kwa rais wa zamani nje ya nchi yake kufuatia makosa alioyafanya wakati wa utawala wake. Wakili wa Habre Mbaye Sene, amesema wamesikitishwa na uamuzi huu na wanaenda kukata rufaa.

 Wakati hukumu hiyo ikitolewa na mahakama maalum nchini Senegal dhidi ya rais huyo wa zamai wa Tchad Hissene Habre mwenye umri wa miaka 73, wananchi nchini Tchad walipewa fursa ya kusikiliza moja kwa moja kupitia runinga na radio vya taifa.