Habari RFI-Ki

AFCON 2017: michuano ya kufuzu kwa fainali za Afrika, Gabon.

Sauti 10:14
Alama ya Shirikisho la Soka barani Afrika.
Alama ya Shirikisho la Soka barani Afrika. CAF

Habari Rafiki tunazungumzia hatima ya timu za mataifa ya Ukanda wa Afrika mashariki na kati wakati zitakaposhuka dimbani mwishoni mwa juma kucheza mechi za lala Salama za kuwania kufuzu Fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwakani nchini Gabon.Tayari timu za mataifa ya Kenya, Rwanda, na Burundi kwa kiwango kikubwa zimepoteza nafasi ya kufuzu; isipokuwa kwa Nchi ya Uganda, DRC na Tanzania, ambayo itategemea matokeo yake dhidi ya Misri na Nigeria kujua hatima yake.Msikilizaji una maoni gani? Unazungumziaje kiwango kilichooneshwa na timu za ukanda ? Na kwa nini unadhani timu za ukanda huo huwa zinapoteza kwenye michuano kama hii?Ungana na mwandishi wetu Reuben Lukumbuka kusikiliza zaidi.