DRC-JOSEPH KABILA

Wafuasi wa Joseph Kabila washerehekea siku yake ya kuzaliwa

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila © AFP PHOTO/ALAIN WANDIMOYI

Maelfu ya wafuasi wamejitokeza kusheherekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa raisi wa jamuhuri ya demokrasia ya Congo Joseph Kabila kwa kukusanyika jijini Kinshasa ambapo suala la kuwa na kura ya maoni itakayoongeza muda wa raisi huyo kusalia madarakani lilijitokeza.

Matangazo ya kibiashara

Pendekezo hilo ambalo bila shaka litachochea wasiwasi wa upinzani kwamba raisi Kabila ambaye aliingia madarakani tangu kifo cha baba yake 2001, anajiandaa kusalia madarakani kwa zaidi ya kikomo cha mihula miwili ambayo ingetamatika decemba.

Katika kile kinachoripotiwa ni kuonesha uungwaji mkono wa raisi kabila,wafuasi takribani elfu tano walifanya matembezi katika jiji kuu la DRC Kinshasa kabla ya kukusanyika katika uwanja mkubwa kuadhimisha kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwake.

Kumekuwa na mshinikizo mbalimbali kutaka serikali ya jamuhuri ya demokrasia ya congo kuandaa uchaguzi,jambo ambalo serikali imedai haliwezekani kufuatia uhaba wa fedha za kuandaa uchaguzi na muda uliobaki hautoshi.