LIBYA-IS

Mji wa Sirte wapokonywa mikononi mwa IS

Vikosi vinavyounga mkono serikali ya Umoja wa kitaifa ya Libya vikiingia katika mji wa Sirte , ngome ya Islamic State 09 Juni 2016
Vikosi vinavyounga mkono serikali ya Umoja wa kitaifa ya Libya vikiingia katika mji wa Sirte , ngome ya Islamic State 09 Juni 2016 Reuters

Majeshi yanayo shirikiana na serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya jana Jumamosi yamesema yamefanikiwa kurejesha mikononi mwao mji wa bandari wa Sirte uliokuwa mikononi mwa udhibiti wa kundi la Islamic State.

Matangazo ya kibiashara

Kudhibitiwa kwa mji wa Sirte, alikozaliwa Moamer Kadhafi itakuwa pigo kubwa kwa wapiganaji hao wenye msimamo mkali ambao pia wamepoteza maeneo kadhaa nchini Syria na Iraq ambayo walijitangazia kuwa ya Kiislamu.

Vikosi vya Libya pia vimerejesha maeneo ya makazi mashariki mwa Sirte, ambayo kwa mwaka uliopita yamekuwa ngome kuu za kundi la Islamic State katika nchi za Afrika Kaskazini, msemaji wa majeshi, Rida Issa, ameiambia AFP.

Wanajihadi kwa sasa wamezungukwa katika eneo la kilomita za mraba zipatazo tano ndani ya mji wa Sirte ambako wameweka mitego yao ya mabomu isiyo na madhara asema msemaji wa majeshi.

Aidha Issa ameongeza kuwa wakkazi wengi wa mji huo wame kimbia lakini baadhi yao wapatao elfu thelathini wamebaki.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya Martin Kobler jana Jumamosi ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa amefurahishwa na hatua za haraka zilizopigwa na majeshi yanayounga mkono serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya.

Ufaransa pia imepongeza hatua hiyo na kutoa wito kwa pande zinazohasimiana kisiasa nchini Libya kuungana dhidi ya kundi la Islamic State.