KENYA - SIASA

Wanasiasa Kenya, waonywa kutoa matamshi ya kichochezi

Vinara wa upinzani, kutoka kushoto, Moses Wetangula, Raila Odinga na Jonston Muthama mbunge anayehojiwa na vyombo vya usalama
Vinara wa upinzani, kutoka kushoto, Moses Wetangula, Raila Odinga na Jonston Muthama mbunge anayehojiwa na vyombo vya usalama REUTERS/Goran Tomasevic

Wanasiasa wawili wa upinzani nchini Kenya, wanazuiliwa na polisi kwa tuhma za kutoa matamshi ya uchochezi. 

Matangazo ya kibiashara

Mbunge Junet Muhammed na Seneta Johnston Muthama kwa sasa wanahojiwa kwa matamshi waliyoyatoa hapo jana baada ya kujibu tuhuma nzito za mbunge wa serikali Moses Kuria kutaka kuuliwa kwa kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

Muhammed alikamatwa baada ya kumaliza mahojiano maaluma na kituo maarufu cha Televisheni nchini humo leo asubuhi katikati ya jijini la Nairobi.

Seneta Muthama naye alizuiliwa nyumbani kwake alfajiri ya leo ambapo baadae alichukuliwa na maofisa wa upelelezi kwenda kuandikisha taarifa.

Wabunge wengine wanaohojiwa ni pamoja na Aisha Jumwa na Timothoy Bosire.

Vinara wa upinzani Raila Odinga na Kalonzo Musyoka wanasema kukamatwa kwa wabunge wao ni uonevu na kujaribu kugandamiza upinzani.

Siku ya Jumatatu wabunge wa serikali, Moses Kuria, Ferdinand Waititu na Kimani Ngunjiri pia walihojiwa na polisi.

Tume ya uwiano na utengamano ya kitaifa inaishtumu Mahakama kwa kushindwa kuwafutia dhamana wabunge ambao wamerelea tena kutoa matamshi ya kichochezi yanayohatarisha usalama na kutengeneza chuki miongoni mwa raia.