ETHIOPIA-HRW

HRW yanyooshea kidole cha lawama polisi ya Ethiopia

Mazishi ya Dinka Chala, aliyeuawa na vikosi vya usalama vya Ethiopia, kijijini Yubdo, katika mkoa wa Oromia, Desemba 17, 2015.
Mazishi ya Dinka Chala, aliyeuawa na vikosi vya usalama vya Ethiopia, kijijini Yubdo, katika mkoa wa Oromia, Desemba 17, 2015. AFP/ZACHARIAS ABUBEKER

Shirika la kimataifa la Haki za binadamu la Human Rights Watch limetoa ripoti leo Alhamisi Juni 16 kuhusu vurugu mbaya za maandamano ya wanafunzi yanayotokea mara kwa mara nchini Ethiopia, katika mkoa wa Oromia tangu mwezi Novemba.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa shirika hilo la haki za binadamu, watu 400 waliuawa. Wanafunzi walikuwa wakipinga dhidi ya mpango wa upanuzi wa mji mkuu wa Addis Ababa, ambao ulisababisha mashamba ya wakulima kutoka jamii ya Waoromo kupokonywa na serikali. Wanafunzi hao walibaini mara kadhaa kwamba jamii ya Waoromo inadulumiwa haki yao.

Ripoti hii, inayozingatia shuhuda kadhaa, inabaini kwamba "mamia ya watu walikamatwa." Inaeleza ukatili uliyotekelezwa na vikosi vya usalama dhidi ya watu kutoka jamii ya Waoromo, si tu kuvunja maandamano, lakini pia dhidi ya waandamanaji waliokamatwa.

Felix Horne, mmoja wa wahariri wa uchunguzi huu wa Human Rights Watch, amesema kuwa watu waliokamatwa wako katika mazingira ya kutisha. "Tumesikia kutoka kwa watu wengi ambao wamekuwa kizuizini kwa muda mfupi, siku mbili au tatu katika vituo vya polisi. Wengi walipigwa vibao, mateke na ngumi. Watu ha walihojiwa kuhusu suala la kujua watu wanaowaunga mkono, ambao wamekuwa wakiwahamasisha kufanya maandamano dhidi ya mpango wa serikali. Lakini pia tuliwasikiliza watu ambao waliwekwa kizuizini kwa muda mrefu, hasa katika makambi ya kijeshi ambapo walikuwa jela kwa miezi kadhaa. Walitueleza mateso waliyoyapata katika sehemu hizo: walitungikwa, waliwekewa kifaa kizito kwenye sehemu zao za siri, mambo kama hayo. Baadhi yao walishtakiwa, lakini idadi kubwa ya watu ambao bado hawajashtakiwa," amsema Felix Home

Human Right Watch inadai kuwa imewatambua kwa majina zaidi ya watu 300 waliuawa, wengi wao wakiwa wanafunzi. "Kinyume na shutuma za serikali, hatukupata ushahidi kwamba waandamanaji walitumiwa na kile serikali ilichokiita makundi ya kigaidi au vikosi vya kigeni kujaribu kuhatarisha usalama wa nchi hiyo. Moja ya mambo ambayo yalinigusa zaidi wakati wa mahojiano niliyofanya, ni kwamba idadi kubwa ya vijana hawa walikuwa na wazo kwamba maandamano yao yanapaswa kuwa ya amani", Bw Home ameongeza.

Kuendesha uchunguzi huru

Kwa upande wake Felix Horne, jumuiya ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na washirika wa Ethiopia, wanapaswa kuwajibika zaidi ili kuzuia majanga ya aina hiyo kutotokea tena. "Jambo muhimu zaidi ni kufanya uchunguzi huru kuhusu vurugu zilizofanywa na vikosi vya usalama. Wale wote watakaokutikana na hatia wanapaswa kuadhibiwa, bila kujali hadhi zao, " Felix Home amesema.