MISRI

Wachunguzi nchini Misri wamekipata kisanduku cha sauti

Mfano wa kisanduku cha sauti kutoka kwenye moja ya ndege zilizoanguka, hiki ni kisanduku ambacho huenda wachunguzi wa Misri, wamekipata
Mfano wa kisanduku cha sauti kutoka kwenye moja ya ndege zilizoanguka, hiki ni kisanduku ambacho huenda wachunguzi wa Misri, wamekipata REUTERS/Hyungwon Kang/File Photo

Kisanduku cha sauti kutoka kwenye ndege ya shirika la Misri "EgyptAir", iliyoanguka mwenzi uliopita, kimepatikana kwenye bahari ya Mediterrania, wamesema maofisa uchunguzi wa Misri.

Matangazo ya kibiashara

Meli iliyokuwa na kifaa maalumu chenye uwezo wa kufika chini ya bahari, imekuwa ikifanya ukaguzi kwenye eneo la bahari ya pwani ya kaskazini mwa Misri, ambapo kifaa hichi kulipiga picha zilizoanishwa na na wataalamu kama kisanduku cheusi cha sauti.

Ndege namba MS804 ikitokea Paris kwenda jijini Cairo, ilianguka ikiwa na abiria 66, ambapo mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika na uchunguzi bado unaendelea.

Moja ya ndege ya shirika la Misri, inayofanana na ile iliyoanguka mwezi mmoja uliopita
Moja ya ndege ya shirika la Misri, inayofanana na ile iliyoanguka mwezi mmoja uliopita REUTERS/Amr Abdallah Dalsh

Awali watengenezaji wa ndege aina ya Airbus, walisema kuwa kupatikana kwa kisanduku cheusi cha sauti kutoka kwenye ndege hiyo, itakuwa ni hatua muhimu itakayosaidia kujua ni kitu gani hasa kilitokea hata ndege ya Misri ikapoteza mawasiliano kwenye rada.

Kupatikana kwa kisanduku hiki cha sauti, kitawasaidia wachunguzi kusikia kile ambacho rubani mkuu na msaidizi wake walikuwa wakizungumza, na ikiwa kuna sauti zozote zilikuwa zinasikika kabla ya ndege kuanguka.

Wachunguzi wanasema kuwa licha ya kupata kisanduku hicho cha sauti, watafutaji walikipata kikiwa kimeharibiwa kwa sehemu kubwa, lakini wamefanikiwa kupata kifaa maalumu ambacho kinatunza sauti, na sasa kitawasaidia kujua kilikuwa kinarekodi nini kwenye kompyuta ya ndege.