DRC-LAMBERT MENDE

DRC: viongozi watembela Kamina baada ya makabiliano

Mji mkuu wa DRC, Kinshasa.
Mji mkuu wa DRC, Kinshasa. Wikimedia/Moyogo

Ujumbe muhimu wa Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umetembelea mji wa Kamina ambako kulitokea mapigano Jumatano wiki hii kati ya askari na wapiganaji wa zamani waliorejeshwa katika maisha ya kiraia, baada ya kuzuka kwa maandamano.

Matangazo ya kibiashara

Matokeo ya vurugu hizo: mtu mmoja, ambaye ni afisa wa polisi aliuawa, watu wanane kujeruhiwa, ikiwa ni pamoja na wapiganaji wanne wa zamani waliorejeshwa katika maisha ya kiraia, kwa ujibu wa serikali alisema. Ripoti hii imepingwa na mashirika ya kiraia ambayo wamebaini kwamba, angalau watu tisa, ikiwa ni pamoja na askari watatu walipoteza maisha katika vurugu hizo.

Kwa upande wake Waziri wa Mawasiliano, Lambert Mende, wapiganaji wa zamani waliorejeshwa katika maisha ya kiraia walikosa hawakuwa wavumilivu. Maandamano haya hayakuwa yanaeleweka, amesema Bw Mende.

"Kulitokea hali ya uvumi kwa upande wa wapiganaji wa zamani waliorejeshwa katika maisha ya kiraia, ambao hawakuvumilia mpango wa kurudishwa katika maeneo yao ya asili, mpango ambao umechelewa kutangazwa. Afisa wa pilisi ambaye alikua kijaribu kujadiliana nao aliuawa kwa kupigwa mapanga, hali ambayo ilisababisha tukio hilo baya kabisa. Kwa sasa hali ya utulivu imerejea baada ya kutangaziwa mchakato wa kurejeshwa makwao kwa makundi, " Bw Mende amesema.

Kundi la kwanza linatarajiwa kurejeshwa katika mikoa yao ya asili mwanzoni mwa wiki ijayo, kwa msaada wa Tume ya Umoja wa Maitaifa nchi Congo (MONUSCO), ameahidi Msemaji wa serikali. MONUSCO inasema iko tayari kutoa msaada wa vifaa. Lakini kwa upande wake shirika la Bill Clinton for Peace Foundation, linasema licha ya idadi iinayotolewa na serikali ni ya uongo, lakini mchakato wa kuwarejesha wapiganaji wa zamani katika maisha ya kiraia umeingiliwa na kasumba kutokana na ukosefu wa nia njema na usimamizi mbovu.

"Walikuwa wakipinga dhidi kutendewa vibaya, walikua hawapatishiwi chakula, walikuwa wametelekezwa," amesema Emmanuel Cole, mkuu wa shirika la Bil Clinton for Peace Foundation mjini Kinshasa. Shirika hili limetolea wito serikali lakini pia jumuiya ya kimataifa kuweka haraka iwezekanavyo mpango sahihi wa kuwarejesha wapiganaji wa zamani katika maisha ya kiraia na kuwakutanisha na familia zao.