MISRI - MORSI

Morsi ahukumiwa kifungo cha maisha jela, 6 kunyongwa

Aliyekuwa kiongozi wa kiislamu, Mohamed Morsi, akiwa mahakamani hivi karibuni.
Aliyekuwa kiongozi wa kiislamu, Mohamed Morsi, akiwa mahakamani hivi karibuni. AFP PHOTO / STR

Mahakama nchini Misri, imemuhukumu kifungo cha maisha jela, aliyekuwa rais wa Kiislamu, Mohamed Morsi, katika kesi ya uhaini iliyokuwa ikimkabili, huku wenzake 6 wakihukumiwa kunyongwa.

Matangazo ya kibiashara

Mahakama imemuondolea Morsi, mashtaka ya kuisaidia nyaraka za siri nchi ya Qatar, lakini ikamuhukujmu kifungo cha maisha jela kwa makosa ya kuongoza mtandao haramu, mwanasheria wake Abdel Moneim Abdel Maksoud, amesema.

Morsi pia amehukumiwa kwa makosa ya kuiba nyaraka za siri zinazohusu usalama wa Misri, ambapo kwenye makosa haya amehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela.

Nchik ya Qatar ilikuwa mshirika wa karibu wa rais Morsi na ilikuwa inaunga mkono Serikali yake na chama chake cha Muslim Brotherhood wakati akiwa madarakani kati ya mwaka 2012 na July 2013 wakati jeshi lilipompindua.

Morsi amehukumiwa adhabuj ya kunyongwa kwenye kesi nyingine tofauti, kutokana na ushiriki wake wa kujaribu kuvunja gereza na kushambulia maofisa wa Polisi mwaka 2011 wakati walipkuwa wakifanya harakati za kumuondoa madarakani Hosni Mubarak.

Aliyekuwa rais wa Misri, Mohamed Morsi akiwa mahakamani hivi karibuni.
Aliyekuwa rais wa Misri, Mohamed Morsi akiwa mahakamani hivi karibuni. DR

Mahakama pia imemuhukumu kifungo cha maisha jela na kifungo cha miaka 20 kwenye kesi nyingine tofauti.

Siku ya Jumamosi mahakama ilithibitisha adhabu ya kifo dhidi ya watuhumiwa wengine 6, wakiwemo waandishi wa habari watatu waliohukumiwa wakiwa hawapo mahakamani wakituhumiwa kutafsiri nyaraka za siri kwa utawala wa Qatar.

Waandishi hao wa habari wametambuliwa kama, Ibrahim MOhame Hilal na raia wa Jordan Alaa Omar Mohamed Sablan, wote wa kituo cha Aljazeera chenye makao yake nchini Qatar.

Mtu wa tatu amefahamika kama Asmaa Mohamed al-Khatib, ripota wa kike aliyekuwa mfuasi wa vuguvugu la Muslim Brotherhood.

Hukumu ya kifo imetumwa kwa mufti mkuu wa Misri kwaajili ya kuzipitia na kuidhinisha ikiwa watu hao wanyongwe au la. Kwa mujibu wa sheria za Misri, adhabu ya kifo inatekelezwa baada ya kupata mtazamo wa wa Mufti mkuu.