DRC-WAHAMIAJI

Maiti 19 za waethiopia zapatikana mpakani DRCongo

Wakimbizi raia wa Ethiopia wakisubiri mashua za kuwasafirisha kuelekea Ughaibuni,2010
Wakimbizi raia wa Ethiopia wakisubiri mashua za kuwasafirisha kuelekea Ughaibuni,2010 AFP PHOTO / TONY KARUMBA

Walinzi wa mpaka wa DRC wamebaini maiti 19 za wahamiaji haramu raia wa Ethiopia waliofariki dunia baada ya kusongamana ndani ya lori.

Matangazo ya kibiashara

Raia 76 walipatikana wakiwa hai katika eneo la kusini mashariki mwa DRCongo ndani ya lori hilo lenye namba zinazoonesha kusajiliwa nchini Zambia.

Msimamizi wa kituo cha mpakani kwa upande wa DRC jimboni Katanga Jean-Pierre Lubosha, ameeleza kuwa lori hilo lilisimamishwa kwa ajili ya ukaguzi kufuatia harufu kali iliyokuwa ikitoka katika lori hilo.

Hata hivyo wamiliki waliwaambia maafisa ukaguzi kuwa walikuwa wamebeba samaki.

Manusura wote walieleza kuwa walikuwa wakielekea Afrika kusini kwa kupitia nchini Kenya kwa lengo la kusaka maisha mazuri.