CAR-USALAMA

Mashambulizi ya waasi yahatarisha utoaji misaada CAR

Wapiganaji wa Seleka katika mji wa Bambari,nchini Jamuhuri Afrika ya kati Mei mwaka 2014.
Wapiganaji wa Seleka katika mji wa Bambari,nchini Jamuhuri Afrika ya kati Mei mwaka 2014. REUTERS/Goran Tomasevic

Dereva wa shirika la madaktari wasio na mipaka MSF nchini Jamuhuri ya Afrika ya kati ameuawa katika shambulizi lililolenga msafara wa shirika hilo.

Matangazo ya kibiashara

Watu waliokuwa na silaha walishambulia msafara huo kati ya eneo la Sibut na Grimari katikati mwa nchi hiyo,ikiwa ni mwezi mmoja baada ya kuuawa kwa afisa mwingine wa shirika hilo kaskazini mwa nchi hatua iliyofanya shirika la MSF kusitisha huduma zake katika eneo hilo.

Thierry Dumont, mkuu wa shirika la misaada nchini Afrika ya kati ameiambia Radio France Internationale kwamba bado sababu ya kushambuliwa haijaweza kufahamika.

Hata hivyo amedai kuwa malori au misaada ya kibinadamu vimelengwa kiuchumi kwakuwa hubeba bidhaa na pesa kidogo.

Taifa la Jamuhuri ya Afrika ya kati ilitumbukia katika machafuko mapema 2013 baada ya waasi wa kiislamu Seleka kumpindua kiongozi aliyekuwa madarakani na kusababisha ulipizaji kisasi kutoka kwa waasi wa kikristo waliojiita Anti balaka.