CAR-MINUSCA

CAR: hali bado tete Bangui

Askari wa MINUSCA kutoka Senegal wakipiga doria katika mitaa ya Bangui Desemba 10, 2015.
Askari wa MINUSCA kutoka Senegal wakipiga doria katika mitaa ya Bangui Desemba 10, 2015. © MARCO LONGARI / AFP

Askari polisi sita wametekwa nyara mjini Bangui na makundi ya wanamgambo ya kata ya PK5. Operesheni imeanzishwa Jumatatu hii Juni 20 dhidi ya wanamgambo wa kundi hilo. Mapigano kati ya polisi na kundi hili imesababisha mamia ya watu kuyahama makazi yao

Matangazo ya kibiashara

Milio ya risasi imesikika katika eneo linalokaliwa na Waislamu la PK5 Jumatatu hii 20 Juni, kufuatia operesheni iliyoendeshwa na vikosi vya kitaifa na kimataifa.

Jumapili mchana, askari polisi sita wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati walitekwa nyara katika katika kata ya PK5. Jumatatu hii mchana, mazungumzo yamefanyika pamoja na watekaji nyara, lakini hawakufikia maelewano.

Baada ya mazungumzo hayo kushindwa, kulisikika milio ya risasi, ambapo mashahidi wanasema ilikua ubadilishanaji risasi kati ya vikosi vya usalama na wanamgambo waliohusika na utekaji nyara wa askari polisi hao. Kwa mujibu wa chanzo polisi, mapigano hayo yamesababisha vifo vya watu watatu.

Kwa mujibu wa mashahidi, askari wa minusca wameshiriki katika mapigano hayo. Watu wanaeleza kuwa operesheni hiyo ilikuwa inalenga wanamgambo wa kundi hilo linaloendesha harakati zake katika kata ya PK5 walioteka nyara askari polisi.

Wakazi wa mtaa wa3 na wa 5 kulikosikika milio ya risasi wamelazimika kukimbilia katika maeneo salama ya mji wa Bangui. Shughuli zimezorota kufuatia hali hiyo. Helikopta za vikosi vya kimataifa zilikua zikipaa juu ya anga ya jiji la Bangui.

Waziri wa Usalama wa Raia, Jean-Serge Bokassa, amethibitisha utekaji nyara huomateka. Ameomba "watekaji nyara kuwaachilia huru mateka hao katika muda mfupi uwezekanao."