DRC-VYOMBO VYA HABARI

DRC: mgomo dhidi ya kupanda kwa bei za matumizi ya intaneti

Bei ya ya matumizi ya intaneti kwa simu imepanda DRC, kabla ya kurudi kwa bei ya zamani kutangazwa.
Bei ya ya matumizi ya intaneti kwa simu imepanda DRC, kabla ya kurudi kwa bei ya zamani kutangazwa. AFP PHOTO / PAPY MULONGO

Mashirika ya vyombo vya habari nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vimetoa wito wa kufanya mgomo Jumatatu hii dhidi ya kupanda kwa bei ya matumizi ya intaneti.

Matangazo ya kibiashara

Vituo vyote vya redio na televisheni vimetakiwa kutorusha matangazo yao ispokua tu kazi za dharura, huku raia wakitakiwa kutoweka salio kwenye simu zao za mikononi. Wito huo Umoja wa kitaifa wa vyama vya waandishi wa habari, Chama cha Waandishi wa habari wa mashirika mbalimbali ya habari, vyombo vya habari binafsi matangazo na. mashirika hayo yanasema hayakubaliani na uamuzi wa serikali wa kupandisha ghafla bei ya matumizi ya intaneti kati ya 35% na 500%. Lakini vyombo vya habari vya Congo, ambavyo vimesema kusononeshwa na hatua hiyo, vimepata ushindi wa kwanza. Mamlaka ya kuchunguza upashaji habari na mawasiliano nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (ARPTC) ilitangaza jana katika taarifa yake kwamba iliyaomba mashirika yanayotoa huduma za inateneti kurudi kwenye bei ya zamani.

Taarifa hii iliyotolewa na Makamu wa Waziei Mkuu mwenye dhamana ya Mawasiliano imerushwa na imekua ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii. Kwenye akaunti yake ya Twitter, Thomas Luhaka ameandika "asante kwa uaminifu wenu". Hakutoa maelezo zaidi. Makamu waziri Mkuu ndiye aliomba uchunguzi na kwa Mamlaka hiyo ya kuchunguza upashaji habari na mawasiliano, kuhusu kupanda kwa beiambayo imezua hali ya sintofahamu, amesema Thomas Luhaka.

Mwingine ambaye ametoa maoni yake, kwenye kmtandao wa kijamii wa Facebook, ni Mbunge kutoka vyama vinavyounga mkono utawala wa Kinshasa, Patrick Muyaya. "Huu ni ushindi wa pamoja, ushahidi wa jinsi tunaweza kufanya kwa pamoja," ameandika Mbunge ambaye alihoji serikali katika kikao cha Bunge.

Maofisa kadhaa wa vyombo vya habari, hata hivyo, walisema jana usiku kwamba kamwe hatafuta uamuzi wao wa kufanya mgomo wa kusitisha matangazo ya vituo vyao redio na televisheni Jumatatu hii ili "kuweka shinikizo kwa mashirika ya nayotoa huduma za intaneti." Pamoja na kwamba, kama alivyosema Patient Ligodi, mmoja wa waanzilishi wa tovuti ya habari ya POLITICO, uamuzi huu wa ARPTC ni ushindi wa uhuru wa vyombo vya habari. Ushindi kwa waandishi wa habari lakini pia kwa umma, haki ya kupata habari kupitia vyanzo tofauti.