BURKINA FASO-USALAMA

Makabiliano kati ya raia katika wilaya mbalimbali Burkina Faso

askari polisi wametumwa katika maeneo yasio salama, Burkina Faso.
askari polisi wametumwa katika maeneo yasio salama, Burkina Faso. © AFP PHOTO / AHMED OUOBA

Mtu mmoja ameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika makabiliano kati ya raia katika wilaya kadhaa nchini Burkina Faso. Makabiliano hayo yaliyotokea ni kati ya wafuasi wa chama kimoja katika baadhi ya maeno na katika maeneo mengine ni wafuasi wa vyama mbalimbali vya kisiasa.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya uchaguzi wa madiwani, ni wakati sasa wa uchaguzi wa waku wa wilaya. Hali ambayo imezua mvutano.

Upande wa mashariki ya nchi, hasa katika wilaya ya Kantchari, makabiliano kati ya pande mbili yamesababisha kifo cha mtu mmoja na watu kadhaa waliojeruhiwa. "Hali hii haikubaliki," Waziri wa Usalama wa Ndani amesema kwenye televisheni ya umma.

Katika jimbo la Karangasso-Vigué, karibu kilomita 400 magharibi mwa mji mkuu, kiongozi mmoja aliyechaguliwa alishambuliwa na watu wanaopinga uchaguzi wake. kiongozi huyo amejeruhiwa na ameruhusiwa kulazwa katika hospitali ya Bobo-Dioulasso, mji wa pili wa nchi ya hiyo.

Moussa Diallo, Meya mpya wa manispaa ya Gomboro, magharibi mwa nchi, alipigwa mawe na waandamanaji. Majengo ya manispaa ya mji yameteketezwa kwa moto. Hali ambayo haivumiliki, ameongeza Waziri. "Wanachoma ofisi ya manispaa ya mji kwa kumchagua meya. Ili ahudumu wapi? " Ameuliza Waziri wa jimbo Simon Compaoré.

Askari polisi wametumwa katika baadhi ya maeneo yasio salama, ili kuzuia kutokea kwa hali mbaya.