NIGERIA-USALAMA

Wafanyakazi 5 wa kampuni ya Australia watekwa nyara Nigeria

Soko la Yenagoa,mji mkuu wa jimbo lenye mafuta la Bayelsa, Nigeria.
Soko la Yenagoa,mji mkuu wa jimbo lenye mafuta la Bayelsa, Nigeria. REUTERS/Akintunde Akinleye

Wafanyakazi watano wa kampuni ya uchimbaji madini ya Australia ya MacMahon, chini ya mkataba na kampuni kubwa ya Lafarge Holcim, wametekwa nyara Jumatano, 22 Juni kusini mashariki mwa Nigeria, baada ya kuanguka mikononi mwa watu wenye silaha, polisi imesema.

Matangazo ya kibiashara

Wafanyakazi hao ni pamoja na raia wawili kutoka Australia, Wanigeria wawili na raia mmoja kutoka Afrika Kusini. Dereva wa gari yao ameuawa kwa pigwa risasi.

Kwa mujibu wa viongozi wa Nigeria, kitendo hiki cha utekaji nyara kilitokea asubuhi katika wilaya ya Akpabuyo, karibu na Calabar, mji mkuu wa Jimbo la Cross River. Hakuna kundi lolote kwa sasa, ambalo limedai kuhusika na kitendo hikii.

Jimbo lenye mafuta

Vitendo vya utekaji nyara kwa ajili ya kupata fidia vimekithiri kusini mashariki mwa Nigeria, jimbo lenye mafuta ambapo makampuni mengi ya kigeni yanaendesha harakazi zao, lakini ni nadra kwa wataalam kutoka nje kutekwa nyara.

Shahidi mmoja, ambaye hakutaka kutajwa jina amesema kuwa wamesafiri na mateka wao katika boti kando na mto unaopita katika jimbo hilo.