DRC-HAKI ZA BINADAMU

Mlipuko wa visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu DRC

Nchini DRC, polisi imesambaratisha mkutano wa upinzani Kinshasa, Mei 26, 2016.
Nchini DRC, polisi imesambaratisha mkutano wa upinzani Kinshasa, Mei 26, 2016. © RFI/Sonia Rolley

Nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kuilishuhudiwa visa vya ukiukwaji zaidi wa haki za binadamu katika kipindi cha miezi mitano mwaka 2016 na mwaka jana. Na mwezi wa Mei kulishuhudiwa visa 155 vya ukiukwaji wa haki za binadamu, Ofisi ya mseto ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu imebaini katika ripoti yake.

Matangazo ya kibiashara

Itakumbukwa kwamba mwezi Mei, upinzani uliitisha maandamano nchini kote. Lakini maandamano hayo yalipigwa marufuku katika mikoa karibu yote ya nchi hiyo.Licha ya marufuku hayo waandamanaji walijaribu kuingia mitaani, laiki polisi iliingilia kati. Hii ndio inajitokeza leo katika takwimu zilizokusanywa na Umoja wa Mataifa.

Visa hivyo ni pamoja hasa na mashambulizi dhidi ya uhuru wa kuandamana kwa amani - angalau maandamano 30 yalizimwa au kufutwa, huku kufuatiwa na mashambulizi dhidi ya uhuru wa kujieleza na kutoa maoni. Kwa mujibu wa ripoiti hiyo, mkoa wa Kivu ya Kaskazini unaongoza, ukifuatiwa na mji wa Kinshasa na mkoa wa zamani wa Katangai.

Hata hivyo Umoja wa Mataifa umesema kuridhishwa na uamuzi wa Mahakama wa kumhukumu askari polisi aliyefyatua risasi kwa kutawanya maandamano ya upinzani ya tarehe 26 Mei wilayani Mbandaka katika mkoa wa Equateur. Askari polisi huyo alihukumiwa kifungo cha miaka 10 jela kwa kosa la kukiuka na kutumia vibaya kifaa cha nchi.

Visa 371 vya ukiukwaji tangu mwezi Januari dhidi ya visa 260 kwa 2015

Pamoja na visa 155 vya ukiukwaji wa haki za binadamu kwa jumla, mwezi Mei unaongoza kwa visa vingi. Kuanzia mwezi Januari hadi mwezi Mei, kulisuhudiwa visa 371 vya ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya visa 260 kwa mwaka mzima wa 2015. Nafasi ya kisiasa inaendelea kupungua nchini DRC, Umoja wa Mataifa umeendelea kusema.

Umoja wa Mataifa umebaini kwamba visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu viliongezeka katika mwezi Mei: visa 384 dhidi ya visa 366 mwezi Aprili. 67% ya visa hivyo havikufanywa na makundi ya waasi, bali na vikosi vya usalama, ikiwa ni pamoja na theluthi moja iliyofanywa na polisi wa taifa.