SENEGAL-KARIM WADE

Karim Wade apewa msamaha na Rais Macky Sall

Karim Wade, mtoto wa rais wa zamani wa Senegal, akituhumiwa kujitajirisha kinyume cha sheria.
Karim Wade, mtoto wa rais wa zamani wa Senegal, akituhumiwa kujitajirisha kinyume cha sheria. AFP PHOTO / STRINGER

Rais wa Senegal Macky Sall amemsamehe Karim Wade na wenzake washitakiwa Ibrahim Abu Khalil na Alioune Samba Diasse. Ofisi ya rais imesema kwamba hatua hii inawaacha wafungwa tu kumaliza adhabu zao, lakini adhabu za kifedha na utaratibu wa kurejesha fedha zilizopitishwa mlango wa nyuma vitatekelezwa.

Matangazo ya kibiashara

Karim Wade, ambaye ni mtoto wa rais wa zamani wa Senegal Abdoulaye Wade alihukumiwa mwaka jana hadi miaka sita jela kwa kosa la kujitajirisha kinyume cha sheria. Amemaliza karibu nusu ya adhabu yake.

Mahakama nchini Senegal ilimuhukumu Karim Wade kifungo cha miaka sita jela na kutakiwa kulipa faini ya Euro milioni 210 kwa kosa la kujitajirisha kinyume cha sheria na hii kufifiza ndoto zake za kuwa mgombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2017.

Licha ya kuondolewa kwa kosa la rushwa katika kesi iliokuwa ikimkabili Karim Wade, mtoto wa rais wa zamani wa Senegal alipatikana na hatia ya kutjitajirisha kinyume cha sheria na hivyo kuhukumiwa kifungo cha mika sita jela na kutakiwa kulipa faini ya Euro miluoni 210

Wakati huo huo mahakama hiyo iliwahukumu kifungo cha miaka mitano jela washirika wa karibu wa Karim Wade hususan Bibo Bourgi, Alioune Samba Diassé, Mamadou Pouye huku wengine wakisafishwa na kuachiwa huru.

katika hali ya kupinga hukumu hii, mwanasheria wa Karim Wade, mtoto wa rais wa zamani wa Senegal Abdoulaye Wade aliamua kukata rufaa katika Mahakama Kuu dhidi ya uamzi wa Mahakama.

Itafahamika kwamba baba wa Karim Wade, ambaye ni rais wa zamani wa Senegal, Abdoulaye Wade, alikua akisema kuwa mwanae anafungwa kwa sababu za kisiasa wala hana hatia yoyote.