AFRIKA KUSINI - ZUMA

Mahakama Afrika Kusini yasema Rais Zuma anaweza kushtakiwa

Jacob Zumam Rais wa Afrika Kusini, ambaye sasa atafunguliwa mashtaka ya rushwa.
Jacob Zumam Rais wa Afrika Kusini, ambaye sasa atafunguliwa mashtaka ya rushwa. REUTERS/Mike Hutchings

Mahakama nchini Afrika Kusini imetupilia mbali jaribio la Rais Jackob Zuma, kukata rufaa kupinga hukumu iliyoagiza afunguliwe mashtaka ya rushwa zaidi ya 800, uamuzi unaoongeza shinikizo kwa kiongozi huyu. 

Matangazo ya kibiashara

 

Rais Zuma alijaribu kupindua uamuzi wa awali wa mahakama wa mwezi April, ya kwamba ofisi ya mwendesha mashtaka ifungue upya mashtaka ya rushwa dhidi yake, yaliyofutwa mwaka 2009, siku chache kabla ya kuwa Rais.

Mashtaka dhidi ya Rais Zuma yanahusu rushwa, udanganyifu, utakatishaji fedha na matumizi mabaya ya fedha za uma, kuhusu ununuzi wa silaha za kijeshi uliogharimu mabilioni ya dola za Marekani.

Rais Zuma amekuwa akipamabana kusafisha jina lake kutokana na tuhuma kadhaa za rushwa zinazomkabili, sambamba na ukosolewaji mkubwa kuhusu sera ya ajira nchini humo.

"Tuliangalia kwa umakini ikiwa rufaa hii ingekuwa na sababu za msingi za kufanikiwa na tumefikia hitimisho ya kuwa hakuna sababu za msingi kwenye hoja zilizowasilishwa." alisema jaji Aubrey Ledwaba wa mahakama kuu ya Pretoria.

Mwaka 2009, ofisi ya mwendesha mashtaka ilitoa maelezo ya kwanini ilimuondolea Rais Zuma mashtaka zaidi ya 700 ya rushwa, ikisema mawasiliano yaliyonaswa wakati wa utawala wa rais Thabo Mbeki hayakuwa na uhusiano wowote kwenye kesi ikiwa wangefungua mashtaka.

Uamuzi huu wa ofisi ya mwendesha mashtaka, ulisafisha njia kwa Rais Zuma, kiongozi wa chama tawala nchini humo cha ANC, kuwania urais wiki chache baadae.wa mahakama unatoa njia kwa Rais Zuma, kiongozi wa chama tawala cha ANC

Mawasiliano yaliyorekodiwa  ambayo yalifahamika kama "Spy tapes" yalifanywa kuwa siri, hadi pala yalipowekwa wazi mwaka 2014 baada ya muda mrefu wa ushindani wa kisheria mahakamani kesi iliyofunguliwa na chama cha upinzani cha Democratic Alliance.

Kwa uamuzik huu, inamaanisha kuwa ofisi ya mwendesha mashtaka itapaswa kumfungulia Rais Zuma mashtaka rasmi ya rushwa, na kumtaarifu tarehe rasmi ya kutakiwa kufika mahakamani.