DRC-UN

UN yapigia kura azimio linaloongeza shinikizo kwa DRC

Jospeh Kabila, rais wa DRC (Desemba 2011).
Jospeh Kabila, rais wa DRC (Desemba 2011). AFP PHOTO / GWENN DUBOURTHOUMIEU

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepigia kura Alhamisi Juni 23 azimio linaloongeza mamlaka ya kundi la wataalam kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kuichukulia vikwazo Serikali ya Kinshasa.

Matangazo ya kibiashara

Vikwazo hivivimeongezwa ili kukabiliana na visa mbalimbali vya ukiukwaji wa haki za binadamu vinavyoendelea kushuhudiwa katika kipindi hiki cha kabla ya uchaguzi.

Onyo la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa Serikali ya Kinshasa liko wazi: Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inaagaliwa kwa ukaribu na Umoja wa Mataifa katika kipindi hiki cha kabla ya uchaguzi. Kama taasisi hii ya kimataifa inaonekana kuwachukulia vikwazo vipya dhidi ya viongozi wa Congo wanaotuhumiwa kutaka kuharibu mchakato wa kisiasa, taasi hii imepigia kura azimio linaloongeza shinikizo kwa serikali ya Joseph Kabila.

Umoja wa Mataifa unaitaka nchi hiyo kufanya uchaguzi kabla ya mwisho wa mwaka huu kwa mujibu wa kalenda iliyoelezwa na Katiba. Umoja wa Mataifa pia una wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa visa vya ukandamizaji, ukiukaji wa haki za binadamu uliofanywa na vikosi vya usalama wa taifa pamoja na mahusiano kati ya makundi ya waasi na mitandao yawahalifui katika utumiaji wa maliasili mashariki mwa nchi hiyo.

Shinikizo juu ya ulinzi wa raia

Lakini azimio linajikita hasa katika suala nyeti: ulinzi wa raia. Mpaka sasa mauaji ya wanawake na watoto tu ndio yalikua yakipelekea kuchukuliwa kwa vikwazo. Kuanzia sasa ukiukaji wa haki zamsingi na haki za binadamu zitapelekea viongozi wao kuchukuliwa adhabu kali.

Visa vya hivi karibuni vya kukamatwa kiholela na utekaji nyara kwa wapinzani vitapelekea Umoja wa Mataifa kufuata msimamo wai serikali ya Marekani ambayo ilipigia kura Alhamisi wiki hii vikwazo dhidi ya mkuu wa polisi katika mji wa Kinshasa, jenerali Célestin Kanyama.