NIGERIA-BOKO HARAM

Jeshi latangaza kuwaokoa mateka zaidi ya 5,000

Wanajeshi wa Nigeria kwenye barabara inayoelekea Chibok, kaskazini-mashariki, Machi 5, 2015.
Wanajeshi wa Nigeria kwenye barabara inayoelekea Chibok, kaskazini-mashariki, Machi 5, 2015. AFP PHOTO/SUNDAY AGHAEZE

Jeshi la Nigeria limetangaza kuwaokoa Jumapili hii, Juni 26 mateka zaidi ya 5,000 kutoka mikononi mwa kundi la Islamic State katika Afrika Magharibi (Boko Haram). Kuokolewa kwa mateka hao ni moja ya matunda ya operesheni iliyoendeshwa kwa ushirikiano wa jeshi, polisi na raia waliojitolea.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa msemaji wa Jeshi ya Nigeria, Kanali Sani Usman, aliyehojiwa kwa njia ya simu Jumapili hii, Juni 26, zoezi la kuwatamu mateka waliookolewa linaendelea. Raia kadhaa waliojitolea watasaidia katika mchakato huu. Lengo lao kuwatokomeza waasi wa Boko Haram.

Hatua hii ya ikikamilika, mateka ambao watakua wametambuliwa watapelekwa katika kambi ya Nema, inayodhaminiwa na taasisi inayosimamia huduma za dharura. Jeshi la Nigeria linasema pia kuwa linashirikiana na mashirika yasio ya kiserikali ya nchini humo na yale ya kimataifa kwa kufanya ukaguzi wa kimatibabu na pia msaada wa kisaikolojia.

Mateka hao wanasadikiwa kuwa zaidi ya 5,000 waliookolewa katika operesheni iliyoendeshwa katika vijiji kadhaa karibu na eneo la Mafa, kilomita arobaini mashariki mwa jimbo la Maiduguri. Jeshi la Nigeria halikueleza kuhusu mazingira yao ya kizuizini.

Wapiganaji kadhaa wa Boko Haram wameuawa katika operesheni hiyo, kwa mujibu wa jeshi la Nigeria. Jeshi hilo limeendelea likisema kuwa askari wa Nigeria walifaulu kukamata magari kadhaa, silaha na risasi za Boko Haram.