MADAGASCAR-USALAMA

Mlipuko wasababisha vifo katika uwanja wa mpira wa Antananarivo

Antananarivo, mtazamo wa uwanja wa mpira wa manispaa wakati wa maadhimisho ya Uhuru Juni 26, 2010.
Antananarivo, mtazamo wa uwanja wa mpira wa manispaa wakati wa maadhimisho ya Uhuru Juni 26, 2010. Afp / Grégoire Pourtier

Watu wasiopungua wawili wameuawa na wengine zaidi ya 80 wamejeruhiwa katika mlipuko wa gruneti uliotokea katika uwanja wa mpira wa mjini Antananarivo, mji mkuu wa Madagascar, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru.

Matangazo ya kibiashara

Jumapili hii, nchini Madagascar, kuliadhimishwa miaka 56 ya uhuru, lakini maadhimisho hayo yalikumbwa na vifo vya watu wasiopungua wawili na wengine wengi kujeruhiwa kufuatia mlipuko uliyotokea katika uwanja wa mpira wa mjini Antananarivo.

Baada ya gwaride iliyoandaliwa asubuhi katika uwanja mkubwa wa manispaa ya Mahamasina, mchana kulikua kulipangwa kufanyika tamasha kabambe ambayo ingeliwakutanisha wasanii nyota wa nchi hiyo na kiingilio ilikua bure. Lakini kwenye saa moja usiku, mlipuko ulitokea katika wa mpira wa mjini Antananarivo katikati ya watu waliokua wakishiriki tamasha hilo.

"Nilikuwa kweny jukwaa. Wakati mlipuko huo ulipotokea, nilihisi kwamba kuna mtu ambaye alirusha bomu lenye mita 10 na sehemu niliyokuwepo, kijana mmoja aliyejeruhiwa katika mlipuko huo ameiambia RFI. Watu waliojeruhiwa walibaki wakigaaga nchini na wale ambao waliweza kuokoa maisha yao walitimua vumbi. Watu watatu miongoni mwa marafiki zangu walijeruhiwa. Na mwingine amefariki papo hapo. "

Wakati huo rais wa Madagascar alitembelea hospitali walikolazwa majeruhi na alitoa rambirambi zake kwa familia za wahanga. Waziri Mkuu kisha alizungumza. "Hiki ni kitendo cha kinyama, aamelaumu Olivier Mahfaly. Damu zimemwagika. mjfikiriye, watu wakirusha gruneti kwa raia wa Madagascar wasio na hatia".

Hata hivyo polisi inasema imeanzisha uchunguzi ili kubainisha watu waliohusika na kitendo hicho kiovu na wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria wahukumiwe kwa mujibu wa sheria.