DRC-USALAMA

Wanamgambo 10 wauawa katika mapigano na jeshi Ituri

Mambasa, Province de l’Ituri, RD Congo. Des policiers congolais en formation à la sécurisAskari polisi wa DRC wakiwa katika mafunzo ya kutoa ulinzi na usalama wa uchaguzi kwa msaada wa MONUSCO. Mambasa, jimbo la Ituri, DRC.
Mambasa, Province de l’Ituri, RD Congo. Des policiers congolais en formation à la sécurisAskari polisi wa DRC wakiwa katika mafunzo ya kutoa ulinzi na usalama wa uchaguzi kwa msaada wa MONUSCO. Mambasa, jimbo la Ituri, DRC. Photo MONUSCO/Anne Herrmann

Wanamgambo 10, wakiwemo wanawake wawili, wa kundi la waasi la FRPI wameuawa na askari wawili kujeruhiwa vibaya katika mapigano yaliyotokea Jumatatu hii Juni 27 katika kijiji cha Kienge wilayani Walendu Bindi kati ya kundi hilo na jeshi.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa vyanzo vya kijeshi, ambavyo vimetoaripoti hii, mapigano yalianza wakati majeshi ya DRC (FARDC) yalipoanza operesheni ya kuvunja ngome za wanamgambo wanaotafuta kujipanga vizuri kwa zaidi ya wiki moja katika mkoa huu wa jimbo la Ituri.

Naibu mkuu wa eneo la kijeshi la FARDC katika jimbo la Ituri amesema kwamba waasi hao wanajaribu kujipanga vizuri ili kuendelea kuhujumu raia.

Baada ya zaidi ya saa tatu ya mapigano, afisa huyo amesema, bunduki tatu aina ya AK 47 zilikamatwa na jeshi na kuwadhibiti wapiganaji wawili.

Chanzo kimoja kinasema kwamba wawili kati ya wapiganaji hao wamejeruhiwa vibaya.

Aidha, vyanzo vya ndani vinaarifu kwamba kundi jingine la wanamgambo liliingia katika kijiji cha Sidabo usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu hii.

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka arobaini amefariki kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kupigwa risasi. Mali kadhaa pia ziliibiwa.