LIBYA-USALAMA-AFYA

Libya: WHO yatoa wito kusitisha mashambulizi dhidi ya hospitali

Wakazi wa Benghazi, karibu na hospitali ya mji, baada ya mlipuko wa bomu lililotegwa ndani ya gari, Juni 24, 2016.
Wakazi wa Benghazi, karibu na hospitali ya mji, baada ya mlipuko wa bomu lililotegwa ndani ya gari, Juni 24, 2016. REUTERS/Stringer

Mwezi Juni kulishuhudiwa mashambulizi matatu yaliyolenga hospitali mbalimbali katika mji wa Benghazi, mji ulio mashariki mwa nchi ya Libya inayokabiliwa na migogoro na migawanyiko.

Matangazo ya kibiashara

Shirika la Afya Duniani (WHO) imelaani mashambulizi ya hivi karibuni yaliyosababisha vifo na majeruhi miongoni mwa wagonjwa na wafanyakazi wa hospitali hizo na kutoa wito kwa pande husika katika vita hivyo kutofanya mashambulizi dhidi ya vituo vya afya. Kwa mujibu wa WHO, karibu 60% ya hospitali na vituo vya afya vinavyopatikana katika maeneo ya migogoro nchini Libya vimefungwa au havihudumu kwa sababu za usalama.

Mashambulizi dhidi ya vituo vya afya yanaendendelea nchini Libya. Athari na na madhara ya mashambulizi hayo vimeendelea kuongezeka. Libya ni nchi ambayo inakabiliwa na migogoro na migawanyiko, huku wanamgambo wakijichukulia sheria mikononi na hawataki kuona vituo vya afya vikifunguliwa au kuheshimu timu za matabibu kutoka hospitali au vituo vya afya. Kusini mwa nchi, kilomita 60 kutoka mji wa Sebha, hospitali moja inatoa huduma za matibabu kwa watu 85,000 katika eneo hilo. Hospitali hii ilikuwa imefungwa kwa siku chache kutokana na sababu za kiusalama. Hata hivyo ilishambuliwa mara kadhaa, lakini kwa mara ya mwisho sio wanamgambo waliotekeleza shambulio dhidi ya hospitali hii.

"Hali ya usalama imekuwa mbaya zaidi siku za hivi karibuni, kama alivyothibitisha Makhzoum Daou, Naibu Mkurugenzi wa hospitali "Baraka el-Shati". Wanamgambo ambao wanajidai kuwa juu ya sheria wakati mwingine wanakuja hapa na kuwapiga matibabu wanaohudumu katika hospitali hii, wageni kama Walibya. Siku chache zilizopita, wakazi wa mji huu walivamia hospitali hii kwa kuweza kuishi emo. Kutokana na hali hiyo tulilazimika kusitisha kazi kwa kusubiri tupate walinzi wenye silaha kwa hospitali. "

Libya, tangu wakati wa Gaddafi, hutegemea wageni katika sekta ya Afya. Idadi kubwa ya matabibu wa kigeni na Waarabu wamekua wakijiuzulu kutokana na hali hiyo. Kwa sasa, Libya inakabiliwa na uhaba mkubwa wa dawa, hasa chanjo kwa watoto.