SUDAN-UNSC-UNAMID

Sudan: UN yaongeza muda wa mwaka 1 kwa Ujume wake Darfur

Askari wa UNAMID akipiga doria katika jimbo la Darfur, Januari 12, 2015.
Askari wa UNAMID akipiga doria katika jimbo la Darfur, Januari 12, 2015. ASHRAF SHAZLY / AFP

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatano wiki hii, limeongeza muda wa mwaka mmoja kwa ujumbe wake (UNAMID) katika jimbo la Darfur, nchii Sudan. Uamuzi ambao umepingwa na Serikali ya Khartoum, ambayo imekua ikiomba kwa miaka kadhaa Umoja wa Mataifa kusitisha kazi ya ujumbe wake katika jimbo la Darfur.

Matangazo ya kibiashara

Kama Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilihakikisha kutozingatia uamuzi huo wa Sudan, limeiomba tena Serikali ya Sudan kuwajibika.

Mitazamo miwili ya mgogoro wa Darfur, ambayo imepelekea Baraza la Usalama kuchukua hatua hiyo. Kwa upande mmoja, nchi za Kiaribu jirani na Sudan kama Misri au Urusia mbazo zilitoa hotuba isiyoeleweka inayokaribisha maendeleo ya usalama katika jimbo la Darfur na kusisitiza haja ya kufikiria mkakati wa kuondoa ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika eneo hilo.

Upande mwengine, nchi za Magharibi ambazo zilibaini kwamba tathmini ya Serikali kuhusu hali ya usalama inayowakabili wakazi wa jimbo la Darfu ni ya uongo. Hivi karibuni, Umoja wa Mataifa ulitangaza kwamba mapigano katika jimbo la kati la Jebel Marra yalisababisha watu 80,000 kuyahama makazi yao tangu mwezi Januari, hali ambayo inakuja kujiongeza kwa watu milioni 2.6 waliohama makazi yao tangu kuanza kwa mgogoro huo.

Baraza la Usalama, hata hivyo, limeweza kukubaliana juu ya azimio jipya la kuongeza muda wa mwaka mmoja kwa ujumbe wake katika jimbo la Darfur (UNAMID), ambapo kipaumbele ni kuwalinda raia na kuwafikishia misaada ya kibinadamu na kuwalindia usalama wa wafanyakazi wa mashirika kihisani. Haya ni masharti matatu ambayo mwanadiplomasia kutoka nchi ya Magharibi ambayo ameelezea Serikali ya Khartoum ili kuzingatiwa kuondoka kwa ujumbe wa Umoja wa Matifa katika jimbo la Darfur (UNAMID). Ujumbe ambao unakosolewa vikali kwa kushindwa kuwalinda raia.