SOMALIA-USALAMA

Watu 18 wauawa katika mlipuko Somalia

Hali ya usalama inaendelea kudorora katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu. Watu wasiopungua 18 wameuawa Alhamisi hii baada ya bomu kulipuka na kuteketeza basi walilokuwemo wakisafiri katika mji mkuu wa Somalia.

Askari polisi wa Somalia wakitazama mabaki ya gari ndogo iliyoharibiwa kwa bomu karibu na eneo la mashambulizi ya wanamgambo wa Kiislam mjini Mogadishu, Machi 9, 2016.
Askari polisi wa Somalia wakitazama mabaki ya gari ndogo iliyoharibiwa kwa bomu karibu na eneo la mashambulizi ya wanamgambo wa Kiislam mjini Mogadishu, Machi 9, 2016. REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Duru za usalma zinaeleza kwamba shambulizi hilo limetokea katika mji wa Lafole.

Inaarifiwa kuwa bomu hilo lilikua lilitegwa pembezoni mwa barabara lililipua wakati basi lililokua liwasafisha abiria lilipopita eneo hilo. Inasadikiwa kuwa abiria wote wameuawa katika shambulio hilo.

Inaarifia pia kuwa washambuliaji hao walikuwa wakilenga gari la wanajeshi lililokuwa karibu.

Ashambulizi kama hayo yamekua yakitokea katika mji mkuu wa Somalia Mogadisho, na tayari yamesababisha vifo vingi.