DRC-MALUMALU

Kanisa Katoliki latangaza kifo cha Padri Malumalu

Mwenyekiti wa zamani wa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (CENI), Padri Apollinaire Malumalu Muholongu wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Kinshasa, Aprili 16, 2015.
Mwenyekiti wa zamani wa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (CENI), Padri Apollinaire Malumalu Muholongu wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Kinshasa, Aprili 16, 2015. RFI

Askofu wa Butembo-Beni, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Sikuli Paluku Melchisédech, ametangaza kifo cha Padri Malumalu Alhamisi Juni 30 kiliyotokea katika mji wa Dallas nchini Marekani.

Matangazo ya kibiashara

"Tunatoa rambirambi zetu kwa familia ya Padri Apollinaire Malumalu, kwa makuhani wote, kwa waumini wa Kanisa Katoliki la Butembo-Beni na wale wote ambao wamehuzunishwa na taarifa hii ya kusikitisha," imebaini taarifa iliyotolewa na Kanisa Katoliki.

Taarifa ya kifo cha Mwenyekiti wa zamani wa Tume Huru ya Uchaguzi (CENI) imethibitishwa na ndugu yake, Emmanuel Tavulya.

"Padri Apollinaire Malulmalu alikuwa mgonjwa. Aliumwa kwa muda mrefu. Kwa siku ya leo, Mwenye Enzi Mungu kuamua vinginevyo, kinyume na yale ambayo tlikua tukitarajia. Ni kweli kwamba Mungu kampenda zaidi. Padri Malumalu amefariki dunia saa 4:30 usiku (saa za mjini Kinshasa), karibu 10:30 alaasiri, saa za mjini Dallas, " amesema Emmanuel Tavulya.

Alisema kuwa hana maelezo kuhusu mpango wa kuusafirisha mwili wa marehemu na lini mazishi yatafanyika, akielezea kuwa marehemu alikuwa Mkuu wa Dayosisi ya Butembo-Beni na rais wa zamani wa CENI.

"Kwa sasa, nitapendelea kuishia kwa hii habari ya huzuni kwa sababu kutakuwa na maandalizi mazima kwa ajili shughuli hii. Mtapewa taarifa katika masaa au siku za mbele, " Bw Tavulya ameongeza.

Padri Apollinaire Malumalu alikua Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini DRC mara mbili. Kwanza kati ya mwaka 2006 na 2011. Na alikua Mwenyekiti wa tume hiyo wakati wa uchaguzi wa rais na wa wabunge mwaka 2006. Alirudi kuwa Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi mwaka 2013 kabla ya kujiuzulu mwaka 2015 kwa sababu za kiafya. Alikwenda kufanyiwa matibabu nchini Marekani.

Tarehe 1 Juni, balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo nchini Marekani, François Balumuene, alitangaza kifo cha Padri Malumalu kwa vyombo vya habari. Taarifa iliyokanushwa na msemaji wa serikali ya Congo ambaye wakati huo alibaini kwamba mapigo ya moyo wa Mwenyekiti wa zamani wa CENI bado yanasikika.