DRC-KATUMBI

Katumbi: Rais Kabila bado hajajibu maswali ya msingi

Mgombea urais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Moise Katumbi, amesema nchi yake inaelekea pabaya kwa vile Rais Joseph Kabila hajajibu masuala ya msingi yanayofukuta kisiasa nchini humo.

Kiongozi wa upinzani na mgombea urais wa DRC, Moise Katumbi, ambaye amesema rais Kabila hajajibu maswali ya msingi kwenye hotuba yake
Kiongozi wa upinzani na mgombea urais wa DRC, Moise Katumbi, ambaye amesema rais Kabila hajajibu maswali ya msingi kwenye hotuba yake REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo wa upinzani ambaye yuko nje ya nchi kwa sababu za kiafya amesema kuwa, dhamira ya rais kabila ya kuendelea kutojibu baadhi ya masuala yenye utata ni hali itakayiongiza nchi hiyo katika "mgogoro mbaya zaidi ".

Aidha, Katumbi amesema, Rais Kabila hajatumia fursa ya maadhimisho ya uhuru kuwahakikishia wananchi kuhusu nia ya kuondoka madarakani tarehe 19 Desemba na kuitishwa kwa uchaguzi tarehe 20 septemba mwaka huu kulingana na katiba ya Congo.

Mbali na hayo, Katumbi ambaye hivi karibuni alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela katika kesi ya ulaghai, amesema kuwa huo ni "upotoshaji kamili ili kumzuia mgombea urais na kwamba huo ni unyanyasaji ambao hautathiri uamuzi wake.

Siku mbili kabla ya uhuru wa Congo, Rais Kabila Kabange akiwa mjini Kalemie, katika ujumbe wake kwa taifa, alielezea dhamira yake ya kuandaa uchaguzi nchini Congo lakini bila ya kubainisha ni lini uchaguzi huo utafanyika.