ZIMBABWE

Wataalamu: Uchumi wa Zimbabwe uko njia panda

Baadhi ya viongozi wa juu kwenye Serikali ya Zimbabwe, wanakiri kuwa chama tawala nchini humo kimeshindwa kudhibiti hali ya uchumi wa taifa hilo, ambao umeendelea kuzorota huku deni la taifa likiongezeka maradufu.

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni Serikali ilidai kuwa imeomba mkopo kutoka shirika la fedha duniani IMF kujaribu kunusu uchumi wake, wakati hii utawala wa Harare ukipambana kupata fedha za kuwalipa mshahara zaidi ya wafanyakazi wa uma laki 3 na elfu 50

Waziri wa fedha, Patrick Chinamasa ambaye yuko nchini Ufaransa kwa ziara, amekiri nchi yake kukabiliwa na uhaba wa fedha, wawekezaji kujitoa pamoja na baadhi ya sera zake kuwachosha wawekezaji hao.

John Robertson ni mtaalamu wa masuala ya uchumi nchini Zimbabwe, anasema sera kandamizi dhidi ya wawekezaji wa kigeni nchini humo ndio zimechangia kuporomoka kw auchumi wake na wawekezaji kukimbia.

Licha ya hali mbaya ya uchumi na kuongezeka kwa tatizo la ukosefu wa ajira nchini humo, Serikali bado inashikilia msimamo wake kuhusu umiliki wa asilimia zaidi ya sabini kwenye sekta zote nchini humo.