CAR

UN kuchunguza madai ya udhalilishaji wa kingono nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Vikosi vya Minusca vikiwa katika doria mjini Bangui, kabla ya uchaguzi wa rais Januari 2 2016.
Vikosi vya Minusca vikiwa katika doria mjini Bangui, kabla ya uchaguzi wa rais Januari 2 2016. ISSOUF SANOGO / AFP

Umoja wa Mataifa unachunguza madai kwamba askari wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wamewadhalilisha kingono watoto wawili, hayo yakiwa ni madai ya karibuni katika wimbi la kesi za kushtua kuwahi kukumba ujumbe wa Umoja wa Mataifa.

Matangazo ya kibiashara

Madai hayo yanatajwa kuwa ya mwezi Mei na yalifanyika katika mkoa wa kati wa Kemo, msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane D  ujarric amesema jana Ijumaa.

Ingawa msemaji huyo hakutoa maelezo zaidi kuhusu idadi ya askari waliohusika au utaifa wao, lakini vikosi vya askari kutoka Gabon na Burundi ndio wanaofanya kazi katika mkoa wa Kemo kama sehemu ya kikosi cha Umoja wa Mataifa MINUSCA.

Umoja wa Mataifa unapanga kutoa taarifa kwa mataifa wanachama wa wanajeshi waliohusika na kuwaomba kupeleka wachunguzi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati ili kusaidia kupata ukweli.

Afisa wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa mmoja wa waathirika wa udhalilishaji huo ana umri wa miaka 12 na mwingine ana umri chini ya miaka 18.