ISRAEL-UGANDA-BENJAMIN NETANYAHU

Benjamin Netanyahu ziarani Uganda

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akiwa na mwenyeji wake rais wa Uganda, Yoweri Mseveni kwenye uwanja wa ndege wa Enttebe, Julai 4, 2016
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akiwa na mwenyeji wake rais wa Uganda, Yoweri Mseveni kwenye uwanja wa ndege wa Enttebe, Julai 4, 2016 REUTERS/Presidential Press Unit/

Miaka 40 iliyopita, Israel ilikumbwa na mashambulizi ya kigaidi, lakini barani Afrika. Utekaji nyara katika uwanja wa Entebbe nchini Uganda, ambapo ndege ya shirika la ndege la Air France ilikua ilitua baada ya kutekwa nyara na Wapalestina wawili na Wajerumani wawili wa mrengo wa kushoto.

Matangazo ya kibiashara

Kikosi cha askari mashuhuri cha Israel kiliingilia kati na kufaulu kuwaua watekaji nyara watatu waliuawa. Miongoni mwa wahanga wa operesheni hiyo, pia kulikuwa ndugu wa Waziri Mkuu wa Israel, Binjamin Netanyahu, Luteni Kanali Yonatan Netanyahu. Miongo minne baadaye, Waziri Mkuu wa Israel ameamua kufanya ziara ya kikazi katika mji mji wa Entebbe.

Ndege ya Benjamin Netanyahu imetua mapema mchana huu na hisia ni kubwa katika uwanja wa ndege wa Entebbe. Ni katika uwanja huo ambapo kulitokea mashambulizi ya kababbe, miaka 40 iliyopita, mashambulizi ambayo yalipelekea matekaa kadhaa wanaokolewa kutoka mikononi mwa kundi la watu wanne waliokua wakiwashikilia mateka. Pia ni wakati muhimu sana kwa Waziri Mkuu wa Israel kwa sababu ndugu yake, Yonatan Netanyahu, alikuwa miongoni mwa askari wa Israel waliowaokoa baadhi ya mateka na aliuawa usiku wa Julai 4, 1976.

Watu 500 wameoalikwa. Miongoni mwao, baadhi ya askari walioendesha operesheni hiyo na mateka waliokua walitekwa nyara.

Benjamin Netanyahu haiko barani Afrika kwa ajili ya maadhimisho hayo pekee. Anakuja kwa kuzungumzia biashara na mapambano dhidi ya ugaidi. Mazungumzo kati ya Benjamin Netanyahu na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni yanaatazamiwa kifanyika mwishini mwa mchana huu, baada ya maadhimisho ya Entebbe.Mazungumzo hayo yatajikita hasa katika swala la usalama, utalii na biashara.

Hatimaye, Waziri Mkuu wa Israel atahudhuria mkutano wa kikanda kuhusu ugaidi, ikiwa ni pamoja na tishio la wanamgambo wa Kiislam wa Al Shebab katika ukanda huo. Watakuwepo katika mkutano huo marais wa Kenya na wa Rwanda. wakati mwingine muhimu kwa Binjamin Netanyahu ni kujaribu kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia na bara la Afrika.