NIGER-USALAMA

Mabomba ya mafuta na gesi yalengwa na mashambulizi Nigeria

Waasi katika jimbo lenye utajiri wa mafuta la Niger Delta nchini Nigeria, limedai kutekeleza mashambulizi matano katika mabomba ya mafuta na gesi katika eneo hilo.

Waasi katika jombo lenye utajiri wa mafuta wa MEND, Nigeria.
Waasi katika jombo lenye utajiri wa mafuta wa MEND, Nigeria. AFP/PIUS UTOMI EKPEI
Matangazo ya kibiashara

Tangu mapema mwaka huu, waasi hao wamekuwa wakishambulia mabomu hayo kwa vilipuzi kushinikiza kugawana mapato yanayopatikana kutokana na rasilimali hiyo.

Ongezeko la shambulizi hili limesababisha hasara na kuanza kuyumbisha uchumi wa Nigeria kwa mujibu wa Benki kuu, wakati huu nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta ikiendelea kukabiliana na ukosefu wa mapato kutoka katika sekta ya mafuta.

Nigeria ni moja ya nchi za Afrika magharibi ambazo zinazokosa usalama kutokana na makundi mbalimbali ya waasi, hususan kundi la Boko Haram, ambalo limekuwa likihatarisha usalama katika nchi za Chad, Nigeria, Cameroon na Niger.