CAMEROON-UFARANSA

Cameroon: mwanasheria Mfaransa Lydian Yen Eyoum aachiliwa huru

Picha ya mwanasheria Mfaransa mwenye asili ya Cameroon Lydian Yen Eyoum iliyopigwa 2014.
Picha ya mwanasheria Mfaransa mwenye asili ya Cameroon Lydian Yen Eyoum iliyopigwa 2014. AFP PHOTO / YEN-EYOUM FAMILY

Lydian Yen-Eyoum, mwanasheria Mfaransa mwenye asili ya Cameroon, ameeachiliwa huru Jumatatu Julai 4, wanasheria wake wamesema. Lydian Yen-Eyoum alikamatwa nchini Cameroon mwezi Januari 2010 na kutuhumiwa kosa la ubadhirifu.

Matangazo ya kibiashara

Alihukumiwa kifungo cha miaka 25 jela na Mahakama Maalum katika sakata ya Operesheni Sparrowhawk, mpango wa kupambana na rushwa ambao ulipelekea kukamatwa kwa viongozi wengi nchini Cameroon.

"Lydian Yen-Eyoumalituita kwenye simu kwa sauti ya furaha akituelza mateso aliyoyapata katika kipindi chote cha miaka sita alichoishi jela. Alitueleza kuwa msimamizi wa gereza alimwambia: " Haya njo uchukuwe vifaa vyakouondoke, " amesema wakili Christian Charriere-Bournazel, mmoja wa waushauri wake.

Rais wa Cameroon Paul Biya alitangaza Jumatatu kwamba amempunguzia kifungo Lydienne Yen-Eyoum. Mwanasheria huyu Mfaransa mwenye asili ya Cameroon alikamatwa mwezi Januari 2010, na alihukumiwa kifungo cha miaka 25 jela Septemba 26, 2014 na Mahakama Maalum kwa kupitisha mlango wa nyuma faranga za Cameroon bilioni 1,077 (sawa na Euro milioni 1.5).

Kwa upande wa wanasheria wake kutoka Ufaransa, wamekaribisha uamuzi huo wa kuachiliwa huru kwa mteja wao. Lydian Yen-Eyoum alikuwa alimaliza rufaa zote za kisheria. Tarehe 9 Juni 2015, Mahakama Kuu, mahakama ya juu nchini Cameroon, ilithibitisha adhabu yake.

Kuachiliwa huru kwa Mwanasheria huyu ni matokeo ya mazungumzo ya kidiplomasia, kwa mujibu wa wakili Christian Charriere-Bournazel mmoja wa washauri wake. "Tulichokua tukisubiri tangu miezi kadhaa, baada ya hivi karibuni kupokelewa katika Ikulu ya Elysée na Bi Le Gal, Mshauri wa Rais, sasa kimefanyika kwa njia ya ajabu kabisa kwa sababu hakuna mtu alijua kama tungelisubiri miezi sita, mwaka mmoja, miaka miwili" , Charriere-Bournazel amesema.

Lydian Yen-Eyoum alikua akikiri kuwa hana hatia. Tayari alikua amesha tumikia kifungo chake kwa miaka zaidi ya sita jela.