DRC-MAUAJI

Miili kadhaa yagunduliwa katika mto Ndjili Kinshasa

La rivière Ndjili qui traverse Kinshasa en RDC.
La rivière Ndjili qui traverse Kinshasa en RDC. Wikipédia

Waathirika wa makundi ya wahuni ya mitaani, ulipizaji kisasi au mauaji yanayotekelezwa na maafis wa serikali? Hayo ni maswali ambayo wakazi wa mji wa Kinshasa wamekua wakijiuliza baada ya miili kadhaa ya watu kugunduliwa Jumapili asubuhi katika mto Ndjili.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mamlaka ya manispaa ya Limete, aina hii ya ugunduzi ni ya kawaida. Wakazi wa mji wa Kinshasa wanaona kuwa miili ya watu iliyogunduliwa ni vijana kutoka makundi mbalimbali ya watu anaona kazi ya jirani makundi.

Miili yote ilikua na majeraha, huku nyuso zikivimba kwa baadhi, mkono kuvunjwa kwa mmoja wao na nguo kuchanika. Papo hapo, familia moja imemtambua mtu wao ambaye anajulikana kwa jina la utani Junior. Kijana wa miaka 22 ambaye, kwa mujibu wa wazazi wake, alikua akiishi katika wilaya ya Lemba. Alitoweka tangu Jumatano na katika mifuko yake ya suruwali kulikua na faranga za Congo 500 na simu mbili za mkononi.

Wafanyakazi wa shirika lisilo la kiserikali "Amour et Verite" na wale wa shirika la Msalaba Mwekundu la DRC walikwenda eneo la tukio baada ya kupata taarifa kutoka kwa mashahidi. Kwa msaada wa mashirika haya, miili ya watu hao ilipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali kuu ya Mama Yemo, baada ya taratibu za polisi.

"Tukio la kawaida," amesema Douglas Nkulu, Meya wa wilaya ya Limete. Kwa mujibu wa kiongozi huyo, tukio hilo ni hutokea mara kwa mara katika katika mto huo unaotokea katika mkoa wa Kongo Central, na ambao umekua ukipeleka watu na wanyama. Lakini baadhi ya wakazi wa mji wa Kinshasa wamenyooshea kidole kundi la wahuni wa jijini hapo wanaojulikana kwa jina la KULUNA, ambalo limeanza kujihusisha na maovu mbalimbali.