COTE D'IVOIRE-ICC-GBAGBO

Kesi ya Gbagbo yaendeshwa faraghani

Rais wa zamani wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo Januari 28, 2016, akisikilizwa kwenye Mahakama ya Kimataifa mjini The Hague (Uholanzi).
Rais wa zamani wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo Januari 28, 2016, akisikilizwa kwenye Mahakama ya Kimataifa mjini The Hague (Uholanzi). ICC-CPI

Hatimaye kesi ya Laurent Gbagbo na Charles Ble Goude inafanyika katika faragha. Majaji wameamua kutorusha tena moja kwa moja hewani vikao vya kesi hiyo wakati ambapo watakua wakisikilizwa mashahidi.

Matangazo ya kibiashara

Mashahidi 13 pekee ambao wamesikilizwa katika kipindi cha miezi sita wameanza kuwa na hofu ya usalama wao.

Wakati kesi ya Laurent Gbagbo na Charles Ble Goude ikianza kusikilizwa tena mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu tarehe 6 Julai, watumiaji wa mitandao ya kijamii na intaneti wa Cote d'Ivoire waliamua kujishughulisha na shughuli nyingine, baada ya kesi hiyo kutoruhusiwa kurushwa moja kwa moja hewani kwenye intaneti. Uamuzii huo ulichukuliwa na majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) tarehe 16 Juni.

 

Charles Blé Goudé, mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), Oktoba 2 mwaka 2014.
Charles Blé Goudé, mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), Oktoba 2 mwaka 2014. ICC-CPI

Vikao vya kesi hiyo wakati wa kusikilizwa mashahidi havitaweza tena kurushwa tena moja kwa moja hewani kwenye intaneti kwa minajili ya kuwalinda mashahidi, lakini vikao vya kesi hiyo vitarudi kurushwa moja kwa moja hewani wiki chache baada ya kusikilizwa kwa mashahidi. Wale waliokuwepo katika ukumbi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) mjini Hague watafuata kesi hiyo baada ya uchunguzi wa kiusalama.

"Hatua hizi zitazuia uwezekano kwa umma kufuata moja kwa moja kesi hii, amesema jaji mkuu Cuno Tarfusser, lakini hatua hizi ni majibu ya matendo ya baadhi ya watu ambao hawawakilisha watu wote wa Cote d'Ivoire lakini ambao wanaonekana kuwa ni tishio kubwa kwa uadilifu wa kesi hii na kwa ajili ya usalama wa mashahidi. " sababu: mahahidi wanaonatakiwa kulindwa wamekuwa wakitambuliwa kwenye mitandao ya kijamii na katika vyombo vya habari vya Cote d'Ivoire. Kwa upande wa majaji, "hali ya mazingira imekua kama kile tunachoamini kuwa ni njia pekee ya kuhakikisha na kudumisha uadilifu wa kesi hii kwa kuhifadhi matangazo ya jinsi kesi inavyoendelea."