DRC-MAUAJI

Miili iliyogunduliwa Ndjili: Ofisi ya mashitaka yaanzisha uchunguzi

Mwendesha Mashtaka Mkuu katika Mahakama ya Rufaa ya Kinshasa / Matete ameanzisha uchunguzi ya miili ya watu iliyogunduliwa Jumapili Julai 3 katika Mto Ndjili.

Mto Ndjili unaopita katika mji wa Kinshasa, DRC.
Mto Ndjili unaopita katika mji wa Kinshasa, DRC. Wikipédia
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa ushahidi uliyokusanywa kutoka kwa wakazi eneo hilo, miili saba iligunduliwa na wavuvi katika Mto huo.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali mtaani Matete, Idumbu Meli Meli, amesema miili ya watu watatu ndio imegunduliwa badala ya saba.

Amesema kuwa maafisa wake walipewa taarifa na raia waliogundua miili hiyo.

"Tulipewa taarifa na raia wema. Papo hapo afisa wa Mahakama waliplekwa katika eneo hilo kama sehemu ya ugunduzi wa miili. Ilibainika kweli kwamba miili ya watu watatu iliondolewa katika Mto. Miili hii mitatu ilikua ilishaanza kuoza, " Idumbu Meli Meli amesema.

Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali amesema kwamba miili ya watu watatu imehifadhiwa kwa sasa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali kuu mjini Kinshasa.

Idumbu Meli Meli anasema polisi inayohusika na masuala ya kisayansi imeanzisha uhunguzi ili kujua sababu za kifo cha watu hawa.

"Tunachunguza mkasa huu. Kwa sasa, kesi imefunguliwa kwa mara ya kwanza katika Ofisi ya mashitaka ya mjini Kinshasa, yenye makao yake Matete, " Bw Meli Meli ameelezea.