LIBYA-SAIF

Mtoto wa Gaddafi Saif al-Islam yuko huru?

Saïf al-Islam Kadhafi, Aprili 27, 2014.
Saïf al-Islam Kadhafi, Aprili 27, 2014. MAHMUD TURKIA / AFP

Raia wa Libya wamechanganyikiwa kuhusu kuachiliwa huru kwa Saif al-Islam Gaddafi, mtoto wa Kanali Muammar Gaddafi, ambaye alikamatwa nchini Libya mwaka 2011 na kushikiliwa mikononi mwa kundi moja la wanamgambo katika mji wa Zintan kusini magharibi mwa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Wanasheria wake ndio wametangaza kuachiliwa kwake, lakini taarifa kutoka pande mbalimbali zinatofautiana.

Kwa mujibu wa afisa mmoja wa kundi hilo la wanamgambo katika mji wa Zintan, Saif al-Islam alikabidhiwa viongozi wa jimbo la Tobruk. Mwanasheria mmoja aliye karibu na familia ya Gaddafi amehakikisha kwa upande wake kwamba Saif al-Islam bado yupo katika mji wa Zintan lakini katika kizuizi cha nyumbani. Lakini kwa sasa, hakuna taarifa zaidi zilizotolewa juu ya tarehe ya uwezekano wa kuhamishwa sehemu nyingine.

Kwa sasa, hakuna kitu kinachothibitisha kwamba mtoto wa Muammar Gaddafi ameachiliwa huru, kama ilivyotangazwa na wanasheria wake Jumatano Julai 6. Tangu Juni 27, wanasheria hao walikua wakiomba kuachiliwa huru kwa Saif al-Islam ambaye Muammar Gaddafi alikua akimchukuliwa kama mrithi wake.

Ombi la kusamehewa lapingwa

Mwezi Aprili uliyopita, Waziri wa Sheria wa Serikali ya Tobruk aliandika barua ya kuomba kuachiliwa kwake kwa niaba ya msamaha wa jumla. Lakini tangu kifo cha Waziri huyo mwezi Juni, ukweli wa barua hii umepingwa. Ni kwa uamuzi huu ambao wanasheria wa Saif al-Islam wanazungumzia kuwa mteja wao yuko huru.

Kwa upande wake, Msemaji wa Bunge la Libya lenye makao yake mjini Tobruk hajathibitisha taarifa hii, lakini pia hajakana. "Hakuna kilio rasmi kwa wakati huu," ameiambia RFI. Fathi al-Maryami amethibitisha hata hivyo kwamba Saif al-Islam anahusika na msamaha wa jumla uliyotangazwa na serikali mwezi Julai 2015. Kwa hiyo ni miongoni mwa watakaoachiliwa huru.

Mwezi Julai 2015, Saif al-Islam alihukumiwa kifo na mahakama bila ya yeye kuwepo, kwa kushiriki katika mgogoro wa mwaka 2011. Pia anatuhumiwa uhalifu dhidi ya ubinadamu na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), ambayo kwa mara kadhaa iliomba asafirishwe.