DRC-SIASA

DRC: Mwanasiasa wa upinzani aliyehukumiwa jela miaka 17 aachiliwa huru

Maandamano ya kupinga marekebisho ya katiba mwaka 2015 mjini Goma
Maandamano ya kupinga marekebisho ya katiba mwaka 2015 mjini Goma Wordpress

Mwanasiasa wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jean Ernest Kyaviro aliyekamatwa na kuzuiliwa kwa kupanga maandamano kupinga marekebisho ya Katiba mwaka uliopita ameachiliwa huru.

Matangazo ya kibiashara

Chama hicho cha RCD-KML kimesema kimefurahishwa na hatua ya kuachiliwa huru kwa mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 48 aliyekamatwa mjini Goma baada ya kufanyika kwa maandamano ya kupinga jaribio la rais Joseph Kabila kutaka kubadilisha katiba.

Akizungumza na Shirika la Habari la Ufaransa la AFP, mke wa mwanasiasa huyo Aline Engbe amesema pamoja na kufurahishwa na hatua hiyo, afya ya mumewe ni mbaya sana.

Katibu Mkuu wa chama hicho Vincent Mumberto amemwambia mwandishi wa RFI Kiswahili Reuben Lukumbuka kuwa mwanasiasa huyo alikamatwa kwa sababu za kisiasa kwa serikali kuhofia umaarufu wake mjini Goma.

Mahakama mwaka uliopita ilimhukumu Kyaviro maisha jela lakini baadaye ikapunguza hukumu hiyo hadi miaka 17 jela kabla ya kuachiliwa huru.