INDIA-MSUMBIJI-USHIRIKIANO

Narendra Modi azuru Msumbiji

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi  ziarani Msumbiji.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ziarani Msumbiji. ISNA

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ameanza ziara yake barani Afrika, akianzia nchini Msumbiji. Kabla ya kuanza ziara hii, Waziri Mkuu Modi amedokeza kuwa anakuja barani Afrika kutoa ujumbe kuwa India ni rafiki wa kuamini.

Matangazo ya kibiashara

Nchini Msumbiji amekutana na rais Filipe Nyusi jijini Maputo na kutoa saini mikataba kadhaa ya ushirikiano wa kibiashara kati ya mataifa hayo mawili.

Wachambuzi wa maswala ya uchumi wanasema ziara ya Modi ni kuyashawishi mataifa ya Afrika kushirikiana na nchi yake zaidi latika maswala mbalimbali lakini pia kuonesha kuwa inaweza kushinda na China ambayo inaonekana kukita mizizi katika matifa mbalimbali ya Afrika na kufadhili miradi kama ya ujenzi wa reli ya kati nchini Kenya na barabara.

Mbali na Msumbiji, Waziri Mkuu huyo atazuru Afrika Kusini, Tanzania na hatimaye nchini Kenya.

Katika ziara hii, kiongozi huyo anatarajiwa kukutana na raia wa India wanaoshi katika nchi hizo ambao ni wengi katika mataifa anayozuru.

Ziara hii inakuja baada ya Waziri Mkuu wa Israel kutamatisha ziara yake barani Afrika hivi leo baada ya kuzuru Uganda, Kenya, Rwanda na kutatishia nchini Ethiopia.