SUDANI-KUSINI-SALVA KIIR

Sudan Kusini kuadhimisha miaka 5 ya uhuru

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (katikati), wakati wa kutia saini kwenye mkataba wa amani Juba, Agosti 26, 2015.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (katikati), wakati wa kutia saini kwenye mkataba wa amani Juba, Agosti 26, 2015. AFP PHOTO/ CHARLES LOMODONG

Sudan Kusini itaadhimisha miaka mitano ya Uhuru wake kesho Jumamosi wakati ambapo hali ya usalama inaonekana tulivu katika baadhi ya maeneo, lakini mapigano yamekua yakirindima katika mji wa Wau.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, serikali ya Juba tayari imetangaza kuwa hakutakuwa na shamrashamra zozote hapo kesho lakini rais Salva Kiir atalihotubia taifa.

Ni miezi michahache tu baada ya nchi hiyo kuanza kushuhudia amani baada ya Rais Kiiir na aliyekuwa kiongozi wa waasi Riek Machar kuanza kushirikiana kuongoza serikali ya mpito.
Nchi hiyo kwa sasa inakabiliwa na chanagamoto za kifedha baada ya miaka miwili ya mapigano lakini mapigano mapya yameripotiwa katika mji wa Wau hivi karibuni.

Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini kimesema kwamba kumekuwa na milio ya risasi zaidi katika mji wa kaskazini magharibi wa Wau.

Inaarifiwa kwamba takriban watu laki mbili unusu wameyahama makazi yao na kukimbilia kwenye maeneo salama.