SUDANI KUSINI-UNSC

Machafuko Juba: UN yaomba mataifa ya Ukanda kusaidia

Wanajeshi na askari polisi wa Sudan Kusini wakitoa ulinzi katika mtaa mmoja mjini Juba tarehe 10 Julai, wakati ambapo machafuka yaukumba mji mkuu.
Wanajeshi na askari polisi wa Sudan Kusini wakitoa ulinzi katika mtaa mmoja mjini Juba tarehe 10 Julai, wakati ambapo machafuka yaukumba mji mkuu. REUTERS/Stringer

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekuatana kwa dharura Jumapili hii Julai 10 kujadili hali ya usalama nchini Sudan Kusini, huku mapigano makali yakiukumba mji mkuu wa nchi hiyo, Juba, kwa siku tatu mfululizo.

Matangazo ya kibiashara

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa wito kwa kurudi kwa hali ya utulivu haraka iwezekanavyo. Baraza hilo limeomba mataifa ya Ukanda kusaidia ili machafuko hayo yakome mara moja.

Marekani ndio wameomba mkutano huo wa dharura. Wanachama 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamekubaliana juu ya taarifa inayolaani vurugu za hivi karibuni, hasa mashambulizi dhidi ya raia.

Mkuu wa oparesheni za kulinda amani, Herve Ladsous, hata hivyo, amesema katika mashauriano yake ya faragha, kwamba tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) haina uwezo wa kuhakikisha majukumu yake ya ulinzi kwa raia kutokana na vurugu zenye kiwango kikubwa.

Kwa hiyo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetuma ujumbe wa nguvu wa kisiasa kwa pande zinazohasimiana nchini Sudan Kusini. Baraza hilo limeweka wazi katika taarifa yake kuwa vikwazo vinaweza kuchukuliwa dhidi ya vikosi vya usalama vitakavyokutwa na hatia ya unyanyasaji dhidi ya raia na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa.

Wiki chache kabla ya kurejelea upya mamlaka ya tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), mabalozi pia wamebaini haraka kinachohitajika kufanywa: kuimarisha mamlaka ya UNMISS, kuongeza wafanyakazi na uwezo wa kutosha.

Katika taarifa yake, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa wito kwa nchi za Ukanda kuwa tayari kutuma askari zaidi wa kulinda amani nchini Sudan Kusini.

Hayo yakijiri maelfu ya watu walikimbia mapigano ya Jumapili. Baadhi walijihifadhi katika kambi ya Umoja wa Mataifa mjini Juba, ambayo tayari inawapa hifadhi karibu wakimbizi 30,000 na ambayo imelengwa mara kadhaa kwa risasi na mabomu. Wengine wamepewa hifadhi katika kambi ya Umoja wa Mataifa, karibu na uwanja wa ndege. Tangu kuanza kwa mapigano, Alhamisi, Julai 7, wakazi wanasalia makwao.